Yanga Yajifungia Hotelini, Kumsajili Hassan Kessy wa Nkana

KAMPUNI ya GSM iliyochukua jukumu la usajili Yanga kwenye msimu ujao, imemuwekea kitita cha Sh 50Mil, beki wa pembeni wa Nkana Rangers ya Zambia, Hassan Kessy.

 

Beki huyo ni kati ya wachezaji wanaowaniwa na Yanga katika kuiimarisha safu ya ulinzi ya kulia pamoja na beki wa KMC, Kelvin Kijiri ambaye klabu yake inahitaji Sh 60Mil ili imuachie kutokana na kubakisha mwaka mmoja katika mkataba wake.

Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango ya kukisuka kikosi chao baada ya juzi kutangaza kuachana na wachezaji wake 14 wakiwemo mastaa Papy Tshishimbi, David Molinga, Mrisho Ngassa na Issa Mohammed ‘Banka’.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na GSM wamemuita beki huyo juzi Jumapili usiku na kukaa naye mezani kwa ajili ya kufanya mazungumzo ambayo yalishindwa kufikia sehemu mzuri kutokana na dau kubwa ambalo amelitaka.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa beki huyo ametaka kitita cha Sh 60Mil kabla ya kupunguza kufikia Sh 55Mil kabla ya viongozi hao kumuwekea dau hilo la 50Mil pekee.

 

Aliongeza kuwa mabosi hao wamefikia makubaliano ya kumpa Sh 50Mil na mshahara wa Sh 4Mil, ambao nao ameukataa akitaka Sh 6Mil ya mshahara ili asaini.“Bado muafaka mzuri haujafikia kati ya uongozi wa Yanga na Kessy aliyekuwepo kwenye mipango mizuri ya kurejea tena Jangwani baada ya mkataba wake Nkana kumalizika.

 

“Kikubwa walichoshindwana ni dau la usajili na mshahara pekee lakini mambo mengine kila kitu kinakwenda vizuri, upo uwezekano mkubwa wa beki na uongozi kumalizana ndani ya wiki hii.

yanga

“Kessy yeye awali alikuwa akitaka Sh 60Mil kabla ya kupunguza na kufikia 55Mil ambazo ni nyingi, mabosi wa Yanga wenyewe wapo tayari kumpatia 50Mil na mshahara wa 4Mil ili asaini Yanga huo ndiyo muafaka uliofikia,”alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Kessy kuzungumzia hilo alisema kuwa “Nipo kwenye mazungumzo mazuri na Yanga kama mambo yakienda vizuri nitasaini mkataba, nisingependa kuweka wazi dau la usajili ambalo mimi nilitaka kwani hiyo ni siri yangu na klabu.”

NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)