NDOA anayotarajia kufunga mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imeibua mambo mazito, huku akihusishwa na msanii wake, Zuhura Othman ‘Zuchu’. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Diamond au Mondi alitangaza kufunga ndoa Oktoba 2, mwaka huu ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (birthday). UTAMU UNAKUJA, UNAKATA Chanzo kutoka ndani ya familia ya Mondi kimedai kwamba, kuna shinikizo kubwa kwa jamaa huyo kutoka kwa baadhi ya ndugu ambao wanamtaka amuoe Zuchu, jambo ambalo linaleta utamu na furaha ndani yao. Lakini wapo ambao wanachukizwa mno na taarifa au shinikizo hilo la Mondi kutakiwa amuoe Zuchu, hivyo hao ndiyo wanakata kabisa utamu wa tukio hilo. VUGUVUGU LA MONDI KUMUOA ZUCHU Vuguvugu la Mondi kutakiwa kumuoa Zuchu, lilianza muda mfupi tu baada ya Aprili 8, mwaka huu, pale mrembo huyo aliposainiwa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Mondi. Baada ya hapo, wawili hao wakawa wanapostiana kwenye mitandao ya kijamii na familia ya Mondi kumsifi ...