Papa Francis awatambua na kuwaridhia maaskofu saba walioteuliwa China
NancyTheDreamtz Makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican na China zimetangaza juu ya kutiwa saini mkataba wa kihistoria, wa muda mfupi uliofikiwa kati ya pande hizo mbili kuhusu uteuzi wa maaskofu nchini China. Papa Francis amekubali uhalali wa maaskofu saba wa China, walioteuliwa na China bila idhini ya Vatican. Hatua hiyo imemaliza mzozo wa kidiplomasia uliokuwepo kwa miongo kadhaa na ambao umesababisha mgawanyiko miongoni mwa waumini wa Kikatoliki nchini China. Ni miongo saba sasa tokea Vatican na China zikate mahuasiano rasmi kati yao. Uamuzi huo ni sehemu ya makubaliano ya kihistoria kati ya Kanisa Katoliki na China juu ya uteuzi wa maaskofu, jukumu ambalo kwa kawaida huwa la Papa. Mkataba huo wa muda ulisainiwa mjini Beijing na kutangazwa wakati Papa Francis alipokuwa anafanya ziara nchini Lithuania ikiwa ni mwanzoni mwa safari yake ya siku nne katika mataifa yanayoizunguka bahari ya Baltic, kaskazini mwa Bara la Ulaya. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vatican, Papa Franc...