Posts

Showing posts from March 10, 2020

Hukumu Ya Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA ni Leo Mahakama Ya Kisutu

Image
NancyTheDreamtz Mahakama ya Kisutu leo March 10, inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi mahakamani hapo. Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018 na Hakimu ambaye sasa ni Jaji, Wilbard Mashauri. Mbali na Mbowe, wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji na Katibu Mkuu wa sasa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na mbunge, Halima Mdee. Wabunge wengine ni Esther Matiko, Esther Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na John Heche. Katika kesi hiyo, baadhi ya washtakiwa waliwekwa mahabusu kwa miezi mitatu kutokana na kukiuka masharti ya dhamana

Aston Villa Ya Mbwana Samatta Yapigwa 4-0 EPL

Image
NancyTheDreamtz KWENYE mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa King Power kati ya Leicester City dhidi ya Aston Villa usiku wa kuamkia leo mambo yamekuwa mazito kwa Villa ya Mbwana Samatta baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0. Harvey Barnes alianza kuitungua Villa dk ya 40 Jamie Vardy alipachika bao la pili dakika ya 63 mkwaju wa penalti kabla ya kurejea tena kambani dakika ya 79 huku mkwaju wa mwisho ukipachikwa na Barnes tena dk ya 85. Aston Villa haikuambulia bao kwenye mchezo huo ambao mabeki walionekana kupoteana mwanzo mwisho. Matokeo hayo yanaifanya Villa kuwa nafasi ya 19 ikiwa imecheza mechi 28 kwenye msimamo ikiwa na pointi 25 na Leicester City kuwa nafasi ya tatu na pointi 53 ikiwa imecheza mechi 29

Jeshi Lathibitisha Mangula Kuwekewa Sumu, Mhusika Kusakwa

Image
NancyTheDreamtz Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, limethibitisha kuwa Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mzee Philip Mangula aliwekewa sumu na uchunguzi wa aliye husika bado unaendelea. Imeelezwa kuwa Mangula alidondoka ghafla mnamo Februari 28, 2020 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM iliyokuwa ikijadiri mambo mbalimbali ya chama likiwemo suala la adhabu ya wanachama watatu. Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa leo Machi 9, 2020, walianza uchunguzi wa tukio hilo baada kupokea taarifa kutoka kwa uongozi wa CCM. “ Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, lilishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na taasisi mbalimbali limebaini kwamba ndani ya mwili wa mzee Mangula kulikuwa na sumu. Uchunguzi kuhusu namna sumu hiyo ilivyoingia mwili wake bado unaendelea kufanyika” imeeleza

Breaking News: Hukumu ya Mbowe, Wenzake Yaahirishwa kwa Muda

Image
NancyTheDreamtz HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, ameahirisha kusoma hukumu ya kesi inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hadi saa 7:30 mchana ambapo tayari watu mbalimbali wamehudhuria kwenye usomwaji wa hukumu hiyo akiwemo Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif. Mahakama hiyo ilitarajiwa leo Machi 10, 2020, kutoa hukumu ya kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wake aliyehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Vincent Mashinji. “Nimefika Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu, Dar es Salaam kusikiliza hukumu dhidi ya viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe ikiwa kuonyesha mshikamano wangu na wa chama cha ACT – Wazalendo katika yale wanayopitia. Pamoja Daima,” amesema Maalim Seif.

Maswali kumi sumu mwilini mwa Mangula

Image
NancyTheDreamtz KAULI ya Jeshi la Polisi kwamba Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula alipewa sumu, imeacha maswali mengi na mjadala mkubwa miongoni mwa jamii. Februari 28, mwaka huu, Mangula alidondoka ghafla katika ofisi ndogo za CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichokuwa kikijadili masuala mbalimbali, ikiwamo adhabu kwa wanachama watatu waliokuwa na tuhuma za ukiukwaji wa maadili ndani ya chama hicho. Katika kikao hicho, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alivuliwa uanachama kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na kanuni ya maadili na uongozi. Tuhuma hizo pia zilikuwa zikiwakabili makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ambaye atakuwa chini ya uangalizi kwa miezi 18 na Yusuf Makamba aliyesamehewa makosa yake. Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema kwa

Floyd Mayweather ‘MONEY’ kuinunua Newcastle United

Image
NancyTheDreamtz Mwanamasumbwi machachari raia wa Marekani, Floyd Mayweather a.k.a ‘Money’ ameonyesha nia yake ya kutaka kuinunua klabu ya Newcastle United inayoshiriki Premier League. Image result for Floyd Mayweather interested in buying Newcastle Bingwa huyo wa dunia, ‘Money’ ameongea hayo wikiend hii iliyopita akiwa kwenye sherehe nyakati za jioni kwenye ‘tour’ yake huko 02 City Hall. Mashabiki wa Newcastle United wamekuwa wakimtaka mmiliki wa klabu hiyo ya England, Bilionea  Mike Ashley kuiuza baada ya uongozi wake wa miaka 13 pasipo mafanikio yoyote. ‘Money’ ni bondia mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, anaaminika kuwa miongoni mwa wanamichezo wanao miliki mkwanja mrefu zaidi. Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 43, katika mapambano 50 aliyopigana ameshinda yote, haja poteza hata moja. Inakumbukwa aliwahi kupigana na nyota wa UFC, Conor McGregor, amewahi pia kupambana na Oscar De La Hoya, Ricky Hatton, Manny Pacquiao na Canelo A