Waraka wa Hamisa Mobetto wagusa Hisia za wengi
NancyTheDreamtz Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameelezea kile anachokabiliana nacho kwenye maisha yake kwa sasa. Hii ni baada ya maneno kuwa mengi mtandaoni kuhusu yeye, sasa ameamua kuvunja ukimya kwa kuandika waraka mrefu kiasi. ==>>Hapa chini tumekuwekea kile alichoandika Hamisa kupitia ukurasa wake wa Instagram; "Pengine hufahamu alipotoka Hamisa Mobetto... Wacha nikufahamishe, nilianza kutambulika rasmi kwenye tasnia ya urembo mwaka 2010 baada ya kuibuka mshindi wa Miss XXL After School Bash. Njia ya mafanikio ilifunguka hapo na hatimae nilishiriki Miss Tanzania na Also Miss New World Tanzania Na Kua first Runner Up 2012. "Lakini Pia Nilifanikiwa Kushriki Miss UniAfrica na kuingia Top Ten... Safari ikaendelea na kwa kuwa urembo ni kipande cha sanaa niliingia kwa pia kwenye Bongo Movie na kucheza filamu kadhaa na huku pia nikiwa Video Vixen kwa baadhi ya nyimbo za Bongo Fleva. "Nisieleweke vibaya kwa hili, kitanda hakizai haramu... ...