Posts

Showing posts from October 29, 2018

Mfahamu mtoto wa kwanza wa Mr Nice, ni mrembo kweli (Picha)

Image
NancyTheDreamtz Mkali wa Takeu Style, Mr Nice Jumatatu hii ameamua kushare kwa mashabiki wake picha ya mtoto wake wa kwanza. Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya shughuli za muziki wake nchini Kenya na Uganda, alipost mtandaoni picha za binti hiyo na baabaye mashabiki wakaanza kumtwanga maswali. “My first lovely queen,” aliandika Mr Nice baada ya kupost picha ya binti huyo. Akijibu maswali ya mashabiki wake, muimbaji huyo alimjibu mmoja kati ya mashabiki wake ambao walitaka kujua kuhusu binti huyo mrembo. Hata hivyo mrembo huyo ambaye anatumia jana la Leylah Mohamed kupitia mtandao wa Facebook, wamewahi kupost picha mbili za baba yake huyo. Related Articles

VIDEO: Zitto aibukia kwenye Korosho na usalama wa taifa ‘Tanzania imekuwa nchi ya watu kutekwa na kushambuliwa kwa risasi’

Image
NancyTheDreamtz Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefunguka ishu ya Usalama wa Taifa la Tanzania kwa sasa na kuzungumzia sakata la Korosho leo Oktoba 28, 2018 kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam. Serikali Imevuruga Zao La Korosho, Imeshindwa Kulinda Ustawi na Usalama wa Raia A: Utangulizi Jana, Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo, ambayo ni Kikao cha Kikatiba ambacho wajumbe wake ni Viongozi wote wa juu wa chama chetu ilikutana katika kikao chake cha kawaida kujadili hali ya chama na hali ya nchi kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine, pia Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo ilitathmini mwenendo wa usalama wa nchi na hali ya Uchumi, hususan masuala yanayohusu wakulima na hasa uzalishaji wa zao la Korosho, zao linaloongoza kwa kuingizia nchi yetu Mapato ya Fedha za kigeni kuliko mazao yote kwa ujumla. Hivyo leo, tumewaita hapa kwa niaba ya Kamati ya Uongozi ili kupitia nyinyi tufikishe...