Posts

Showing posts from February 18, 2020

LIVE: Zitto Kabwe anazungumza na Waandishi wa habari muda huu

Image
NancyTheDreamtz Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe muda huu anazungumza na waandishi wa habari, bonyeza PLAY hapa chini kutazama LIVE. BREAKING LIVE : PIGO KWA MBOWE, MASHINJI APOKELEWA CCM

Kisa Cha SODOMA..Mungu Aliwashushia Mvua ya Moto Kwa Kuendekeza USHOGA...Walitaka Kuwabaka Malaika

Image
NancyTheDreamtz #TheStoryBook #SodomaNaGomorrah  Hadithi kamili ya kisa cha Mji wa Washenzi Sodoma na Gomora, na jinsi Mungu alivyouangamiza kwa moto na kupindua Ardhi Juu chini Tazama VIDEO:

PAUL Makonda Atamani Kigamboni Kufanana na Mji wa Manhattan Marekani

Image
NancyTheDreamtz Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Jumanne Februari 11, 2020 amemuomba ruhusa Rais wa Tanzania, John Magufuli aweze kuifanya Wilaya ya Kigamboni kufanana na mji wa Manhattan uliopo Jiji la New York, Marekani. Makonda ametoa kauli hiyo katika hafla ya uzinduzi wa jengo la manispaa ya Kigamboni na jengo la mkuu wa Wilaya hiyo eneo la Gezaulole Kigamboni. "Niruhusu mheshimiwa Rais kupitia miradi ya maji, umeme, hospitali, barabara niifanye wilaya ya Kigamboni kuwa wilaya ya kisasa". "Tumetembea huko duniani tumeona. Ukienda pale Manhattan, New York City upande wa pili utakuta kuna kisiwa cha Jersey, Kuna mambo mazuri. Haka ndio ka kisiwa ketu kawe na hoteli nzuri za kitalii, fukwe nzuri. Mtu akitaka kwenda kula maisha anasema ni Kigamboni hapana sehemu nyingine," amesema Makonda

Breaking News : Zitto Kabwe Akutwa Na Kesi Ya Kujibu

Image
NancyTheDreamtz Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT – Wazalendo) Zitto Kabwe amekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka matatu ya uchochezi yanayomkabili katika Mahakama ya Kisutu. Zitto amepewa siku nne kuanzia tarehe 17 Machi-20 Machi 2020 kuwasilisha ushahidi wake wa utetezi. Hivyo, Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Machi 17, 18, 19 na 20, 2020 Katika kesi ya msingi, Zitto anabiliwa na mashtaka matatu yote ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28 mwaka 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Kocha simba :Leo tutatoa soka safi kwa mashabiki

Image
NancyTheDreamtz KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa leo watatoa soka safi kwa mashabiki wa Simba mbele ya Kagera Sugar. Simba ina shuka Uwanja wa Taifa, Februari 18 ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya Lipuli uliochezwa Februari 15 Uwanja wa Samora Iringa. Sven amesema:"Wachezaji wapo vizuri na maadalizi yamekamilka kwa ajili ya mchezo wetu, tunaamini tutaoa soka safi kwa mashabiki wetu,". Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 56 baada ya kucheza mechi 22 za ligi na Kagera ipo nafasi ya sita na pointi zake 34.

Mimi ni hazina kubwa, CCM watanilea na ipo tayari kuwaendeleza Watanzania na kule nilikotoka huo utayari siuoni” Dkt. Mashinji

Image
NancyTheDreamtz Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Vicent Mashinji, leo Februari 18, 2020 amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Hamphrey Polepole. Dkt Vicent Mashinji, baada ya kupokelewa katika Ofisi ndogo za CCM, Lumumba Akiwa katika ofisi ndogo za CCM Dkt Mashinji amesema kuwa baada ya kutafakari kwa muda juu ya mwenendo wa siasa nchini, aliona chama cha CHADEMA bado kiko mbali katika kuchochea suala zima la maendeleo ya vitu na watu. “Malumbano ya Asubuhi mpaka Jioni nilikuwa naona yanatuchelewesha, nikaona ni heri nije hapa Lumumba, niongee na wenzangu nione kama nitapata fursa ya kutoa mchango kwenye Taifa langu, mimi bado ni kijana miaka 47 ninaweza nikawa hazina kubwa ambayo CCM kinaweza kikanilea na kunikuza zaidi” amesema Dkt Mashinji. Usiku wa kuamkia Disemba 20, 2019 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, alimpende...