Posts

Showing posts from August 23, 2018

BASATA washikwa kigugumizi kujibu sakata la WCB na Rich Mavoko ‘nyie mmesikia kafukuzwa tayari?’ (+video)

NancyTheDreamtz araza la Sanaa Taifa (BASATA) leo limewakutanisha tena Rich Mavoko na Uongozi wa WCB akiwemo Diamond Platnumz kujadili ishu ya mkataba inayoendelea kati ya msanii huyo na lebo ya WCB. BASATA wameshindwa kueleza kwa kina ni mambo gani waliyoafikiana lakini wamesema wanachojua ni kwamba Rich Mavoko yupo WCB na hajafukuzwa hizo ni ishu za mitandaoni.

Simba Yafungua Ligi Vizuri Yaitandika Tanzania Prison Bao 1-0

Image
NancyTheDreamtz MABINGWA watetezi, Simba wameanza vizuri Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Tanzania Prisons ya Mbeya bao 1-0 katika mchezo uliofanyika usiku huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Bao la Simba limefungwa na mshambuliaji kutoka Rwanda, Meddie Kagere aliyefunga dakika ya pili kwa shuti kali baada ya kupewa pasi na John Bocco kutoka upande wa kulia. Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dillunga/Nicholas Gyan dk82, Meddie Kagere, John Bocco/Adam Salamba dk83 na Shiza Kichuya/Muzamil Yassin dk67. Tanzania Prisons: Aaron Kalambo, Benjamin Asukile, Laurian Mpalile, Nudrin Chona, James Mwasote, Jumanne Elfadhili, Salum Kimenya, Cleophace Mkandala, Kelvin Friday/Lambert Sabiyanka dk82, Salum Bosco/Ramadhani Ibata dk71 na Ismail Aziz/Hassan Kapalata dk79. 

Nuh Mziwanda Afunguka Mazito Kuhusu Mjengo wa Shilole "Mimi Nilichangia Kununua"

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda ameibuka kuwa ana yeye pia aliweka mkono Kwenye kununua Mjengo mpya wa Shilole aliouanika Kwenye mitandao ya kijamii. Ikiwa ni siku chache zimepita tangibly shilole aanikr Mjengo wenye thamani ya zaidi milioni 90 anaoujenga hivi sasa, aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda amedai na yeye pia ana chake Kwenye Mjengo huo.

Watoto wa Mzee Majuto Wafukuka Kuhusu Tuhuma za Kumfukuza Mama Yao

Image
NancyTheDreamtz Siku chache baada ya mke wa marehemu Mzee Majuto, Aisha Yusufu kudai kufukuzwa na familia ya msanii huyo, ndugu wametoa msimamo wao kuhusiana na sakata hilo wakisema wamezisikia tuhuma hizo. Madai hayo yanakuja ikiwa ni siku 15 zimepita tangu alipofariki msanii huyo maarufu wa vichekesho aliywahi kutamba na filamu kama Back From New York, Inye na Mzee wa Chabo. Wiki iliyopita mwanamke huyo alizungumza na vyombo vya habari akidai kwamba baada ya kumalizika kwa shughuli za maziko, ndugu walimwambia aanze kujitegemea kwa kila kitu ikiwemo chakula, jambo ambalo alilitafsiri ni sawa na wamemfukuza. Katika maelezo yake mama huyo wa watoto wanne, amesema ndugu hao walimwambia kwamba ataishi kwa fedha za pole ambazo waombolezaji mbalimbali wameendelea kumpa. MCL Digital ilizungumza na Hamza ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mzee Majuto kwa njia ya simu, ambaye alisema hayupo tayari kuongea kwa sasa hivi lolote juu ya suala hilo mpaka hapo itakapofika siku ya kufanya arobaini. “A...

Idriss Aamua Kupita Njia za Daimond Baada ya Kuwa na Wema Sasa Atoka Kimapenzi na Lynn

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa Bongo movie na comedian maarufu Idris Sultan anadaiwa kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Ex girlfriend wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz. Kumekuwa na tetesi kuwa Video vixen ambaye hakauki vituko Kwenye mitandao ya kijamii Irene Geofrey maarufu kama Lynn ana banjuka na Idris Sultan. Tetesi za Mahusiano ya wawili hao zilianza juzikati ambapo watu wengi walipigia mstari baada ya mwanadada huyo kuposti picha ya Idris huku akiandika maneno ya kimahaba yalisomeka; “Babyboo baby boo bae.” Baada ya Tetesi hizo kupamba moto Kwenye mitandao ya kijamii gazeti la Risasi Vibes, lilimsaka Lynn ambaye mara moja alikana kuwapo kwa Mahusiano hayo: Unajua muda mwingine unaweza kuposti kitu halafu maneno yakajiandika yenyewe, sasa ndicho kilichonitokea na mimi sikutaka kufuta kwa sababu watu wangesema ni kiki. Lakini Idris ni mshikaji wangu wa karibu sana na ninampenda anavyochekesha, watu wasinitengenezee mambo ambayo hayapo jamani“.

Ninja Agoma Kuitumia Jezi ya Can­navaro..... Bado Aiweka Kabatini

Image
NancyTheDreamtz Jezi ya Yanga yenye namba 23 ambayo Nadir Haroub ‘Can­navaro’ alimkabidhi Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aendelee kuitumia baada ya yeye kustaafu kucheza soka, jezi hiyo bado ipo kabatini. Cannavaro ambaye ni meneja wa Yanga kwa sasa, hivi karibuni alitan­gaza kustaafu kucheza soka akiwa nahodha wa timu hiyo ambapo uongo­zi ulitaka kuistaafisha jezi yake, lakini yeye akakataa na kumkabidhi Ninja. Ninja ambaye alisajiliwa na Yanga msimu uliopita, bado hajaanza kuitumia jezi hiyo na wikiendi iliyopita kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger alivaa jezi yake namba 6 aliyokabidhiwa wakati anatua Yanga. Kwa mujibu wa Gazeti la Championi, Ninja amesema jezi hiyo anasubiri kuan­za kuitumia kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu ambao unaanza leo huku Yanga ikicheza ke­sho Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. “Unajua jezi niliyoachiwa na Cannavaro siwezi kuitumia kwenye michuano ya kimataifa kwa sababu kule natam­bulika ninaitumia jezi namba 6, lakin...

Breaking News: Bobi Wine Akamatwa Tena Muda Mfupi Baada ya Kuondolewa Mashtaka

Image
NancyTheDreamtz Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amekamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini. Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa. Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Seebait.com 2018SeeBait Rapper 50 Cent Amsifia Nick Minaj Licha ya Kuchanwa Vibaya na Mrembo Huyo

Image
NancyTheDreamtz Rapper 50 Cent amekuwa wa kwanza kujibu kati ya male rappers kadhaa waliochanwa kiutani na Nicki Minaj kwenye wimbo wake wa hivi karibuni 'Barbie Dreams' kutoka kwenye album ya QUEEN. Kwenye mahojiano na 'Extra' kupitia Hip Hop N More, 50 Cent ameweka wazi hisia zake juu ya wimbo ule kwa kuupa alama 100. Alisema: "Nimeupenda ule wimbo, niliwahi kufanya wimbo unaitwa 'How to Rob' na aliwahi kusema mwenyewe (Nicki Minaj) kuwa alivutiwa nao sana." alisema 50 Cent na kumsifia Nicki kwa uandishi wake wa mtindo wa mtazamo tofauti yaani kinyume (reverse perspective) Aliongeza pia kuwa 'Barbie Dreams' inaonesha wazi kabisa kuwa wanawake kwenye Hip Hop wameanza kuchukua nguvu kutoka kwa wanaume - Swipe kuona interview hiyo. Kwenye dude hilo, 50 Cent alichanwa kwenye line isemayo: "I tried to f k 50 for a powerful hour, but all that ni *a wanna do is talk 'Power' for hours." alichana Nicki. Wengine waliotajwa kwenye w...

Ray C "Wabongo Mitandaoni Wanapenda tu Vitu vya Kijinga vya Maana Holla"

Image
NancyTheDreamtz Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Ray C amedai kwamba asilimia kubwa ya watanzania hawajui kuitumia mitandao ya kijamii ipasavyo ili iwaingizie fedha, na badala yake wanaitumia kwa kujadili mambo yasiyo na tija kwa mtu mwenyewe na taifa kwa ujumla. Ray C ameeleza hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv hii leo Agosti 23, 2018, na kusema watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha zao kuingia kwenye mitandao hiyo bila ya kufikiria ni jinsi gani itaweza kuwarudishia faida. "Watu wengi mitandaoni wanapenda upuuzi, ukiweka kitu cha maana hakuna mtu ambaye ata 'comment' chochote katika hicho ulichokiweka, maana wanakichukulia poa lakini fanye kinyume chake hapo ndio utawajua walipo. Wenzetu Ulaya mitandao ya kijamii kama wakina Kim Kardishian na wengine wanatumia mitandao hiyo kuuza 'product' na kuonyesha kazi zao ili wapate pesa... lakini sisi ndio tumekuwa wakutoa pesa kwa kununua bando ili tukaharibu, tena sana sana Tanzania hatujui kutumia mita...

Young Dee "Ile Gari Nimenyanganywa Haipo Tena Mikononi Kwangu"

Image
NancyTheDreamtz Rapper Machachari Young Dee Ametoboa siri kuwa kwa sasa ile gari aliyoinunua kwa mil 25 haipo mikononi mwake kwani ilinunuliwa na Uongozi aliyokuwa nayo kipindi cha nyumba hivyo wamechukua gari lao Young Dee akihojiwa ameweka wazi kuwa kwa sasa anataka kununua Lambogini kama mambo yakimwendea vizuri Young kwa sasa anakampuni yake inayoitwa Dream City ambayo inasimamia kazi zake pia

Wanaharakati Kenya Waungana Kumpinga Rais Museven wa Uganda

Image
NancyTheDreamtz Nchini Kenya wanaharakati pamoja na wanasiasa wamejiunga na wenzao wa Uganda kushinikiza utawala wa rais wa Yoweri Museveni kuzingatia sheria na kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa. Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema yatawasilisha kesi katika mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuishinikiza serikali ya rais Museveni kuzingatia sheria dhidi ya wafungwa wa kisiasa.

Breaking News: Bobi Wine Akamatwa Tena Muda Mfupi Baada ya Kuondolewa Mashtaka

Image
NancyTheDreamtz Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amekamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini. Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa. Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.