Posts

Showing posts from September 10, 2020

Makala: Urafiki, Aadui wa Osama Bin Laden na Marekani; Al-Qaeda na ‘Ushetani’

Image
Na Josefly “Alikuwa mtoto mwenye sura ya mvuto, mpole na mwenye nidhamu. Ilikuwa nadra kutazamana naye moja kwa moja machoni. Alikuwa na aibu, msikivu na neno lake halikutoka kinywani mwake bila mpangilio,” alisema Bi. Alia Ghanem, mama mzazi wa Osama Bin Laden, aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda akielezea maisha ya utotoni ya mwanaye, miaka nane baada ya kuuawa na makomando wa Marekani waliomsaka kila kona ya dunia kwa kipindi cha miaka kumi. Kwa mujibu wa mama huyo ambaye amebarikiwa kuishi hadi leo, tangu alipomzaa mwanaye Osama, Machi 10, 1957 katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia, aliiona baraka na neema kwenye maisha ya mwanaye. Kila alipokuwa akivuka rika moja, alionesha kuwa na upeo wa hali ya juu. Darasani alikuwa na akili za kipekee na alifanikiwa kumaliza Shahada ya Uchumi kwa ufaulu mzuri katika Chuo Kikuu Cha King Abdulaziz kilichoko Jiddah, Saudi Arabia. Akiwa na umri wa miaka 20, alianza kuonesha makucha ya uwezo wake na alifanikiwa kuwa na ushawishi m

CEO Mpya Simba Ataja Mikakati Yake

Image
MTENDAJI mpya wa Simba, Barbara Gonzalez, ametaja vipaumbele vyake mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuwa mtendaji wa klabu hiyo kwa kusema atahakikisha anaongeza mapato katika klabu hiyo kupitia viingilio ikiwa pamoja na kusimamia timu hiyo kufanya vyema kimataifa. Simba imemtangaza Barbara kuwa mtendaji mpya wa klabu hiyo, hivi karibuni baada ya Senzo Mazingisa kuhamia Yanga ambapo anatarajia kufanya mabadiliko kuelekea msimu mpya wa ligi kuu. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barbara alisema kuwa moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anaboresha uhusiano mzuri kati ya Simba na mazingira yanayoizunguka klabu hiyo. “Moja ya mikakati yangu ni kuhakikisha naboresha uhusiano mzuri wa klabu kwenye vyombo vya habari, kuitangaza klabu ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya klabu kwa ujumla, mimi nitasimamia masuala yote ya klabu na mwalimu yeye atasimamia masuala ya benchi la ufundi, pia nahitaji kuhakikisha naongeza mapato ya uwanjani. “Moja ya kazi ya mwalimu Sven Vandenbroeck anayot