Posts

Showing posts from May 21, 2019

Muna Love "Kazi Yangu Inayoniweka Mjini ni Kufagia Makaburi ya Kinondoni

Image
NancyTheDreamtz MSANII wa filamu ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki wa Injili, Rose Alphonce ‘Muna Love’ amemtolea povu si la nchi hii shabiki wake aliyetaka kujua wapi anapopata fedha za kutanua. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muna alimjibu shabiki anayejiita Anitha_sanga_e ambaye alipoona picha ya Muna mtandaoni humo iliyoonesha anakula bata, ndipo alipomuuliza: “Muna unafanya kazi gani?”  Unataka kujua alijibu nini? Mambo ni moto, hili ndilo lilikuwa jibu lake: “Nafagia makaburi ya Kinondoni mpenzi.”

Nyota Yako Leo Jumanne 21 May 2019

Image
NancyTheDreamtz 🔯NG'OMBE -  (April 21– May 21) Leo hii ukimuona mtu ana ndevu nyeupe, basi ujue hiyo ni ishara ya kuwa mambo yako sasa yatafunguka na kukunyookea, ile mikwamo ya hapa na pale itafunguka kwa urahisi. 🔯MAPACHA - (May 22- Juni 21) Leo katika matembezi yako ukikutana na mwanamme amevaa mkufu wa shanga, hiyo ni dalili ya kupata kila kitu utakachokihitaji bila ya kutumi67a muda au nguvu nyingi.Unashauriwa kuwa mtu wa ibada na kutoa sadaka. 🔯KAA - (Juni 23- Julai 22) Leo Mchana ukikutana na Mwanamme akiwa amevaa Mkufu wa Fedha, hiyo ni dalili ya kutimia kwa ndoto yako ya kupata Mwanamke au Mwanamme mzuri na kutimia kwa Ndoa yako. 🔯SIMBA LEO -  (Julai 24- Agosti 23) Ukimwona mtoto Leo hii analia, basi hiyo ni ishara ya wewe kupata mtoto mzuri au utapata mpenzi mpya ambaye utakutana naye bila ya kutegemea. Sherehe utakayohudhuria itakutanisha na wangu wengi ambao hukutegemea. 🔯MASHUKE - (Agosti 24- Septemba 23) Elewa kuwa ile posa yako imekataliwa na mpenzi un...

Mwanamuziki Rihanna Aamua kuja na Albamu ya Reggae

Image
NancyTheDreamtz Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Rihanna anaanda Albamu ya Reggae, Mwaka jana pia alidokeza lakini akapiga tena kimya. Kupitia mahojiano yake mapya na jarida la ‘NY Times’ Rihanna amethibitisha kuwa anaandaa Albamu ya Reggae, Pia amefunguka kuwa bado hajajua jina la Albamu japo mashabiki wengi wanataka iitwe “R9” kwasababu ni Albamu yake ya 9. Pia alipoulizwa kama ana mpango wowote wa kufanya kazi na Drake alisema sio siku yoyote ya hivi karibuni.

Humphrey Polepole apata uteuzi serikalini

Image
NancyTheDreamtz Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama wa Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, ameteuliwa na waziri wa Ardhi William Lukuvi, kuwa mjumbe wa shirika la nyumba la taifa (NHC). Waziri Lukuvi ameteua wajumbe hao 7 wa bodi ya shirika la nyumba la taifa, leo Mei 20, 2019 siku chache baada ya Rais Magufuli kumteua Dr. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo. Wajumbe walioteuliwa ni, 1. Bi. Immaculate Senye 2. Bi. Sauda Msemu 3. Bw. Abdallah Mwinyimvua 4. Bw. Humphrey Polepole 5. Bw. Martine Madeke 6. Eng. Mwita Rubirya 7. Bw. Charles Singili

Mwanariadha wa kike wa Kenya asema hawezi kupunguza homoni za kiume

Image
NancyTheDreamtz Bingwa wa mbio za mita 800 nchini Kenya kwa upande wa akina dada Margeret Nyairera Wambui amesema kuwa hatotumia dawa za kupunguza homoni za kiume ili kushiriki katika mbio hizo. Akihojiwa na BBC mwanariadha huyo amesema kuwa dawa hizo zina kemikali ambazo huenda zikakuathiri katika maisha ya baadaye. ''Mimi siwezi kutumia dawa kwa lengo la kutaka kupata fedha,Mungu aliniumba niwe hivi nilivyo - kumbuka dawa hizi zina kemikali ambazo madhara yake baadaye huenda yakawa mabaya katika mwili wako. Wakati huo wote IAAF haitakuwa hapo''. Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 24 ni miongoni mwa wanariadha walioathiriwa na sheria mpya ya shirikisho la riadha duniani IAAF inayowataka wanawake walio na viwango vya juu vya homoni za kiume testosterone kutumia dawa ili kuzipunguza mwilini. IAAF inasisitiza kuwa sheria hiyo ni nzuri katika kuleta usawa katika mashindano , ikihoji kwamba wanariadha wenye homoni za kiume wanafaidika kutokana na ongezeko la nguvu kati...

Sylvestre Ilunkamba Achaguliwa Waaziri Mkuu mpya DRC

Image
NancyTheDreamtz Hatua ya Rais Felix Tshisekedi kumteua Profesa Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa waziri mkuu mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo imepokelewa kwa hisia mseto. Uteuzi huo umefanyika baada ya waziri mkuu aliyekuwepo Bruno Tshibala, kujiuzulu. Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi wake alisema waziri huyo mkuu alielezea kipaumbele ya serikali yake itakayoundwa baadaye. ''Rais alinipokea na aliniambia ya kwamba kipaumbele cha serikali hii yetu ya muungano ni ni kuboresha maisha ya raia na kurejesha usalama'' alisema Bw. Illunga. Pia alimshukuru rais wa zamani Joseph Kabila kwa kupendekeza jina lake ali ateuliwe kuwa waziri mkuu. Raia wa Congo walikua wamesubiri zaidi ya miezi mitatu, bila ya kuwa na waziri mkuu mpya. Slyvestre Illunga aliwahi kutumika chini ya utawala wa Mobutu Seseko kama mshauri wake wa maswali ya uchumi. Kutokana na uzoefu wake katika masuala ya uongozi baadhi ya raia wana matumaini kuwa waziri mkuu huyo mpya ataleta m...

Mbunge wa CCM Aitaka Serikali Kuhusu Kilimo cha Bangi Bangi Tanzania

Image
NancyTheDreamtz Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ameishauri Serikali ya Tanzania kuruhusu kilimo cha bangi nchini kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za binadamu. Amesema hayo leo Jumatatu Mei 20, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020. Amesema nchi nne Barani Afrika zimeruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa za binadamu. “Amebainisha dawa nyingi za maumivu ya saratani asilimia 80 zinatokana na bangi, “Nashangaa wataalam wetu wa Mamlaka ya Chakula la Dawa (TFDA) wangekuwa wameshachukua sampuli na wangewajulisha kuwa dawa zilizo na bangi ndani yake.” “Wangemuuliza msambazaji hiyo bangi anaitoa wapi? Spika sisi wenyewe tunayo bangi hiyo tunaona kila siku inakatwa ukweli nyingi sio kwa ajili ya kuvuta. Bangi hiyo imekuwa ikienda katika dawa za binadamu.” Amesema ana ushahidi Lesotho na Zimbabwe kuruhusu ulimaji wa bangi na kuna viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu kwa kutumia bangi. Amesema gunia moja la b...