Posts

Showing posts from August 7, 2018

Mambo sita usiyoyafahamu kuhusu Alikiba na Coastal: Mkataba, namba ya jezi, mchezo wake wakwanza na muziki (Video)

Nancy The Dream Tz iliandika habari juu ya uongozi wa Coastal Union ulitangaza dhamira yake ya kumsajili Alikiba na kumtumia kwenye msimu huu wa mwaka 2018/19 ligi kuu habari ambayo ilizua gumzo ndani na nje ya nchi kwa msanii huyo maarufu Barani Afrika kuamia upande wapili wa shilingi huku wengine wakiamini haiwezekani. Siku nne baadaye Julai 27 klabu ya Coastal Union ikaidhihirishia umma kuwa kila kitu kinawezekana baada ya kutangaza rasmi kumsajili Alikiba ambaye hucheza nafasi ya ushambuliaji ndani ya uwanja,  Bongo5  ilipotoa ripoti hiyo kupitia tovuti na mitandao ya kijamii ikazua gumzo huku mashabiki wa mziki kila mmoja akiandika mtazamo wake. Wakati kwa sasa msanii na mcheza soka nchini, Alikiba akifanya mazoezi ya kujiandaa na kazi yake mpya ambayo ameamua kuitumikia kwa sasa tulipata nafasi ya kumtembelea uwanjani na kujionea ni kwakiasi gani anavyojifua huku tukizungumza na uongozi wa klabu yake ya Coastal Union kujua utaratibu waliyompangia na haya ndiyo mambo...