BINGWA mtetezi wa ligi kuu Simba, leo Juni 19, imefanikiwa kuvuna alama tatu, dhidi ya Polisi Tanzania, kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kushinda bao 1-0. Goli pekee la kwenye mchezo huo limefungwa na Luis Miquissone dakika ya 28 kwa adhabu ndogo (Free kick) baada ya beki wa kulia Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi nje ya 18, bao hilo la nane kwenye ligi kuu kwa ‘Konde Boy’ Kwa matokeo hayo Simba ambaye ni bingwa mtetezi wa ligi imefikisha alama 70, baada ya kushuka dimbani mara 28, nafasi ya pili ipo Yanga yenye alama 64, baada ya kucheza michezo 30. NancyTheDreamtz
Posts
Showing posts from June 20, 2021
Kajala: Paula Anakwenda Shule
- Get link
- X
- Other Apps
S TAA mkali wa Bongo Movies, Kajala Masanja, amevunja ukimya uliotawala kwa kipindi kirefu baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’; kubwa ni suala la mwanawe, Paula Paul au Paula Kajala kwenda shule. Kajala anasema kuwa, kwa sasa yupo fiti na anaendelea vyema na maisha yake kama kawaida. Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA, Kajala ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Paula anasema amekutana na changamoto nyingi ndani ya mwaka huu na kamwe hawezi kuja kusahau ambapo amejifunza mambo mengi maishani mwake. Kajala anasema kuwa, yeye pamoja na mtoto wake, Paula wamejifunza mengi ambayo hawatayasahau. KWANI KAJALA MWENYEWE ANASEMAJE? IJUMAA: Habari za siku kedekede Kajala… KAJALA: Salama...