NancyTheDreamtz Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali, amekiri chama chake kuitumia dola kuhakikisha kinabaki madarakani. Amesema kama chama chochote kinachoongoza serikali kitashindwa kutumia dola kubaki madarakani, utakuwa uzembe wa chama chenyewe. Kwa kulitambua hilo, Dk. Bashiru amesema CCM imekuwa ikitumia dola kujihakikishia ushindi wakati wa uchaguzi na mwaka huu wamepanga "kuitumia dola kweli kweli". Lakini, kiongozi huyo wa CCM akaonya kuwa chama kinachoongoza serikali, hakipaswi kuitumia dola kunyanyasa wapinzani wake. Dk. Bashiru aliyasema hayo katika mahojiano maalum na vyombo vya habari vya IPP alivyovitembelea jijini Dar es Salaam jana. "Ukishakuwa chama tawala, kuna dhana inaitwa nafuu ya mwenye madaraka. Ukishindwa kutumia nafuu hiyo, utakuwa kama KANU (chama tawala cha zamani cha Kenya), iliposhindwa kutumia nafuu hiyo, haikuwahi kurudi madarakani au UNIP ya Zambia. "Unashika dola halafu unatumi...