Kasi ya Kagere Yamuibua Hamissi Tambwe "Kagere ni Moto wa Kuotea Mbali Sitashangaa Akiwa Mchezaji Bora Msimu Huu"
NancyTheDreamtz Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, ameibuka na kusema straika wa Simba, Meddie Kagere ni moto wa kuotea mbali. Ni baada ya Kagere kufunga mabao yote mawili juzi, wakati Simba ikiichinja JKT Tanzania 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Tambwe amesema amekuwa akimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo ambaye alijiunga na Simba Juni, mwaka huu akitokea Gor Mahia ya Kenya. Tambwe amempongeza Kagere kwa kufikia rekodi yake ya kufunga mabao saba katika mechi 11 za kwanza Simba. Alisema, yeye pia msimu wa 2013/14 aliposajiliwa na Simba akitokea Vital’O ya Burundi, alifunga mabao saba katika mechi 11 za kwanza. “Kwa hiyo, Kagere ni mmoja kati ya washambuliaji hatari sana msimu huu na jinsi mambo yanavyoenda, sitashangaa kama ataibuka mfungaji bora. “Ana tofauti kubwa na washambuliaji wengine wa Simba, anafunga Uwanja wa Taifa lakini pia katika viwanja vya mikoani, kwa hiyo nampongeza kwa hilo, lakini pia kitendo chake cha kuifikia rekodi yang...