Posts

Showing posts from October 19, 2019

Samatta atuma salamu za ushindi Taifa Stars

Image
NancyTheDreamtz Nahodha na mshambuliaji wa kikosi cha taifa Stars Mbwana Ally Samatta amewapongeza wachezaji wa timu hiyo, kwa kufanikisha lengo la kufuzu fainali za mataifa bingwa ya Afrika “CHAN” kwa kuifunga Sudan mabao mawili kwa moja mjini Khartoum, jana usiku. Samatta ambaye hakuwepo kikosini hiyo jana kufuatia kanuni za michuano ya CHAN kumnyima nafasi ya kushiriki, ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter. Kanuni za michuano ya CHAN zinawabana wachezaji wanaocheza nje ya ligi za nyumbani kwao kushiriki kwenye vikosi vyao, kwa kusudio la kuwapa fursa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, kuonekana kimataifa. Mshambuliaji huyo ambaye anaitumikia klabu ya KRC Genk ya Ublegiji ameandika, “Heshima kubwa mmetupa watanzania, nasimama kwa heshima, navua kofia yangu nawapigia saluti ya heshima, asante sana @TaifaStars na hongereni kwa kufuzu kwenye michuano ya CHAN 2020, na kama ilivyo ada basi hapo hapo Sudan anzeni kunywa izo koka bili juu yangu