NancyTheDreamtz Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, amesema walimkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang’wale, Geita, Carlos Gwamagobe, akitaka kutoroka kwenda nchi jirani baada ya upotevu wa zaidi ya Sh bilioni 2.2. Kauli hiyo aliitoa jijini hapa jana wakati akifunga mafunzo kwa wakuu wa wilaya wapya 27 na wakurugenzi 39 walioteuliwa Julai na Agosti, mwaka huu na Rais Dk. John Magufuli. “Kwa mfano juzi juzi pale Nyang’wale watu wameiba zaidi ya shilingi bilioni 2.2, sio fedha za mchezo eti mfano Halmashauri ya Kakonko inakusanya shilingi milioni 343,” alisema na kuongeza: “Halmashauri nyingine wameiba shilingi bilioni 2.2 sawa na miaka saba ya ukusanyaji wa Kakonko, lakini muda mfupi watu wamechukua akaunti inasoma ziro. “Halafu hawana shaka wanafunga mikanda, nimpongeze mkurugenzi wa Nyang’wale, alionyesha ndani ya muda mfupi anafaa kuwa mkurugenzi. “Alikataa baada ya kuona vitu havijakaa sawa, angeenda kichwa