Diamond Platnumz Atubu Kwa Hamisa Mobetto Linapokuja Swala la Fashion, Unaambiwa Hamisa Ndo Anamvalisha Mondi

Mwanamitindo @hamisamobetto na mzazi mwenzake @diamondplatnumz waendeleza mahusiano yao kikazi baada ya Diamond kuweka wazi kuwa kampuni ya #MobettoStylish ndio ilihusika kumvalisha siku ya harusi ya @esmaplatnumz na Msizwa

Hii itakuwa kwa mara nyingine tena baada ya @diamondplatnumz kukiri kuvalishwa na kampuni hiyo kwenye show ya Zuchu Mlimani City. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameishukuru kampuni hiyo inayomilikiwa na mzazi mwenzake huyo @hamisamobetto kwa kumvalisha kwa mara ya pili

Hii ni hatua nzuri kwa mastaa hawa ambao wamezaa mtoto mmoja. Hapo awali hawakuwa kwenye mahusiano mazuri baada ya kuanza kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii muda mfupi baada ya kuachana.
NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Waziri Lugola Awaondoa Madarakani Maafisa Wa NIDA Mkoa Wa Ruvuma

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo