Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanayoitia tumbo joto Marekani na washirika wake
NancyTheDreamtz Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya. Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500. Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana. Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani Rais Donald Trump mnamo Februari alitangaza kuwa Marekani itajitoa kutoka mkataba huo iwapo Urusi haitotii, na kuweka tarehe ya mwisho kuwa Agosti 2. Rais wa Urusi Vladimir Putin na yeye amesitisha majukumu ya taifa lake katika mkataba huo muda m