NancyTheDreamtz Karibu kwa ajili ya kujuzwa na pia kupata taarifa (masasisho) mbalimbali ya kile kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus) almaarufu kama "kirusi cha Wuhan" kutoka nchini China. Katika uzi huu utapata kufahamu mambo mbalimbali hususani hali ya ongezeko na ukuaji, jitihada zinazofanyika kukabiliana na kirusi hiki na mengine mengi yanayoibuka duniani kote katika muda wowote kuanzia sasa. Nikukaribishe sana! Coronaviruses in virusi vinavyopatikana zaidi kwa wanyama, lakini katika matukio machache virusi hivyo ninavyoitwa Zoonotic, Kisayansi, vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu. Virusi hivi vinaweza kuwafanya watu wakaugua, mara nyingi katika sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji sawa kabisa na mafua ya kawaida. Virusi husambaa kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine kwa njia ya hewa kwa kukohoa au kupiga chafya, kugusana na mtu mwenye virusi hivyo. Njia nyingine ni kugusa kitu au sehemu yenye virusi na kisha kujigusa mdomo, ...