Posts

Showing posts from December 29, 2018

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Rais Magufuli Kuamuru Kikokotoo cha Zamani Kitumike Mafao ya Wastaafu

Image
NancyTheDreamtz Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe  amempongeza Rais John Magufuli kwa kukubali ushauri walioutoa na kuacha upande wa waziri, washauri wake na watendaji wa Serikali yake. Maoni ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini ameyatoa leo baada ya Rais Magufuli kurejesha utaratibu wa awali wa kikokotoo cha asilimia 50 kwa watumishi wa Serikali na asilimia 25 kwa wafanyakazi wa sekta binafsi. “Kufuatia uamuzi wa Rais Magufuli kuhusu kikokotoo cha mafao ya pensheni kwa wastaafu , sisi ACT Wazalendo na vyama vya upinzani kwa ujumla tumesimama na wafanyakazi toka mwanzo wa sakata hili, wakati sheria ikiwa muswada na hata baada ya kanuni kutungwa,” amesema  “Kwetu, jambo lolote linaloongeza maslahi na ustawi wa wafanyakazi ni jambo jema na muhimu. Tunashukuru kuwa Mheshimiwa Rais ametuelewa na amekuja upande wetu na na kuacha upande wa waziri wake, washauri wake na watendaji wa Serikali yake,” ameongeza.  “Tunapoelekea mbele, tunamuomba asiwe na aibu k

Serikali Yazifunga akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa Korosho Kupisha Uhakiki

Image
NancyTheDreamtz Serikali imefunga kwa muda akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa korosho kupisha uhakiki wa kina wa umiliki wa korosho walizouza. Uamuzi huo unakuja wakati ikiwa imeshaingiza Sh3.8 bilioni kwenye akaunti hizo katika mfululizo wa uhakiki na ulipaji wakulima wa zao hilo unaoendelea nchini. Akizungunza na gazeti la The Citizen, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema wakulima wenye akaunti hizo wameuza zaidi ya kilo 1,500 kwenye vyama tofauti vya msingi, hivyo ni lazima umiliki wa korosho walizouza uhakikiwe. “Hatua hii ni muhimu (ya kufunga akaunti hizi kwa muda) ili kupisha uhakiki kwa sababu utaratibu unataka mkulima aliyeuza zaidi ya kilo 1,500 za korosho aonyeshe shamba lake lilipo kwa timu yetu ya uhakiki,” alisema Hasunga “Lakini uchunguzi wa awali umeonyesha kuna baadhi ya wakulima wameuza kiasi kinachofikia kilo 3,000 za korosho kwenye vyama vya msingi tofauti.” Hata hivyo, waziri huyo alisema Serikali bado haijapata kiasi ha

Walichokisema Sumaye, Zitto Kabwe Baada ya Tundu Lissu Kusema Yupo Tayari Kugombea Urais 2020

Image
NancyTheDreamtz Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamesema wanamsubiri kwa hamu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu apitishwe na chama chake kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020. Lissu anayetibiwa nchini Ubelgiji baada ya shambulio la risasi zaidi ya 30 lililotokea Septemba 7, mwaka jana akiwa Dodoma, juzi aliliambia gazeti la Mwananchi kwamba hatakuwa na kipingamizi ikiwa chama chake kitampitisha kuwania nafasi hiyo. Kauli ya Lissu ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya CCM, imepokewa kwa furaha na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiamini anaweza kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa chama tawala. Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe alisema Lissu atavifaa vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2020. Maoni ya Rungwe yaliungwa mkono na Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alisema hana shida na kauli ya Lissu. “Jambo la muhimu kuliko yote ni kuwa mwaka 2019, kwetu ni mwaka wa kudai demokrasia. Azimio la Zanzibar limeweka mpango ma

Kwa Hili la Mwanamuziki Diamond, Basata Mnajitukanisha Wenyewe

Image
NancyTheDreamtz BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) chini ya katibu mkuu wake, Godfrey Mngereza, ni kama limepoteza mwelekeo. Viongozi wake wamekuwa na ndimi mbilimbili, maamuzi yao hayana nguvu tena na hata umuhimu wake wa kuwepo, haupo. Ukitazama sarakasi zinazoendelea kati ya Basata na wasanii Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) na Raymond Mwakyusa (Rayvanny), kuhusu kufungiwa kwa wimbo wa Mwanza (Nyegezi), unaweza kuwafananisha Basata na mbwa mkubwa asiye na meno, anaishia kubweka tu lakini hawezi kung’ata.  Novemba 12, 2018 (mwezi uliopita), Basata walitangaza kuufungia wimbo wa Mwanza (Nyegezi) wa Rayvann na Diamond Platnumz. Wakati Basata wakitangaza kuufungia wimbo huo kwa sababu za kimaadili, hatua hiyo ilikuwa imekuja kwa kuchelewa.  Unafungiaje wimbo ambao tayari watu wameshaudownload, watu wanao kwenye simu zao, kwenye laptop zao, kwenye vyombo vyao vya usafiri mpaka majumbani mwao? Licha ya kutangaza kuufungia wimbo huo, na kuwakataza wasanii husika kutoupiga sehemu yoyote,

Waziri Jafo Abaini UFISADI Wa Mabilioni Ulanga

Image
NancyTheDreamtz OFISI ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) imebaini matumizi mabaya ya fedha za serikali Sh. bilioni 2.98 katika halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wakuu wa idara wote waliohusika wavuliwe nyadhifa zao huku watumishi wengine waondolewe majukumu ili vyombo vya dola viendelee na hatua kwa mujibu wa sheria dhidi yao. Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Twala za mikoa na Serikali za mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uchunguzi maalum uliofanywa kwa halmashauri ya wilaya hiyo. Jafo alisema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi imefanya uchunguzi maalum katika halmashari 12 nchini ambazo ni Ulanga, Same, Mbulu, Meru, Itigi, Misungwi, Nyang’hwale, Serengeti, Bahi, mpwapwa, Morogoro Dc na Kibaha Tc ambapo katika halamasahuri ya Ulanga uchuguzi ulianza Novemba 13 hadi 23 mwaka huu. Alisema uchunguzi huo ulifanyika kufuatia malalamiko ya wanachi mbalimbali pamoja na mbunge wa jimbo la Ulang

Q-chiller Azimika na Sauti ya Isha Mashauzi.

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa siku nyingi Q-chiller amefunguka na kusema kuwa kila msanii amekuwa na sauti yake na radha yake ya muziki kwa upande wake anaona kuwa moja ya sauti za wasanii zinazomkonga nyoyo ni  sauti ya mwanadada muimbaji Isha Mashauzi. Isha mashauzi ni moja ya wasanii wa kike walioo katika game kwa muda mrefu na wameweza kulinda heshima ya muziki wa taarabu kutokana na sauti yake lakini pia kuipenda kazi yake ya muziki. Q-Chiller amekuwa moja ya wasanii wanaosema wazi sana kuhusu vile wasanii wnegine wamekuwa wakifanya kazi na mafanikio yao pia.

Diamond na mpenzi wake Watinga na Balozi wa Tanzania nchini Comoro

Image
NancyTheDreamtz    Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amekutana na balozi wa Tanzania nchini Comoro.  Katika hafla hiyo Diamond alikuwa ameongozana na mpenzi wake kutoka nchini Kenya, Tanasha. "Earlier today when i visited the Tanzanian Embassy in Comoros," ameandika Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram.