Posts

Showing posts from March 13, 2020

Trump Akataa Kupima Corona ilihali waziri awekwa karantini

Image
× BREAKING NEWS Polisi Yapiga Mabomu Chadema Waliomfuata Mbowe Segerea Breaking News: Corona Yatua Kenya, Mmoja Athibitika CCM Yamnasua Mashinji Jela, Yamlipia Mil. 30 – Video Trump Agoma Kupima Corona, Waziri Mkuu Awekwa Karantini March 13, 2020 by  Global Publishers WAZIRI Mkuu wa  Canada, Justin Trudeau,  na mke wake watabaki kwenye karantini kwa siku 14, baada ya mkewe, Sophie Gregoire Trudeau, kukutwa na virusi vya Corona na ambaye kwa mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano wa Waziri Mkuu, ”anaendelea vizuri na dalili alizonazo si mbaya.” Bwana Trudeau pia atakuwa kwenye karantini kama hatua ya tahadhari. Hatapimwa katika hatua za sasa kwa kuwa haonyeshi dalili za maambukizi. Katika ukurasa wa Twitter, Bi Sophie aliandika ”nitarejea nikiwa na afya njema hivi karibuni.” Bi Trudeau amesema alikuwa amepata dalili ambazo hazikuwa za kawaida na kuongeza kuwa ”kuwa kwenye karantini si kitu ukilinganisha na fa

China wadai huenda Virus vya Corona Vilienezwa na jeshi la USA

Image
NancyTheDreamtz    Na AFP AFISA wa cheo cha juu wa China amedai huenda jeshi la Amerika lilipeleka virusi hatari vya corona nchini humo huku maradhi hayo yakiendelea kuenea mataifa mbalimbali na kuua watu zaidi ya 5,000. Bila kufafanua, msemaji wa wizara ya ulinzi wa China, Zhao Lijian, aliandika kwenye Twitter kwamba, kuna uwezekano virusi hivyo vilipelekwa China na wanajeshi wa Amerika. Dai lake linawiana na habari zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii nchini China zikilaumu Amerika kwa mkurupuko huo. Mkuu wa kituo cha kudhibiti maradhi nchini China amesema, maradhi hayo yalianza soko la Wanyama katika jiji la Wuhan. Hata hivyo, maafisa wa China na wataalamu mashuhuri wa afya wanadai huenda virusi hivyo vilitoka kwingineko. China imefokea maafisa wa Amerika wanaoita maradhi hayo “virusi vya Wuhan.” Kwenye ujumbe wake wa Twitter, Zhao alipakia video ya mkuu wa kituo cha kuzuia maradhi cha Amerika akiwa mbele ya bunge la Congress akisema, baadhi ya raia wa Am