Posts

Showing posts from March 22, 2020

Jinsi Mgonjwa wa Kwanza wa CORONA Alivyoingia Uganda

Image
NancyTheDreamtz Waziri wa Afya wa Uganda, Ruth Jane Aceng alisema kisa hicho kilichothibitishwa ni raia wa Uganda mwenye miaka 36 ambaye aliingia nchini humo akitokea Dubai Jumamosi Machi 21 saa 2 asubuhi kwa ndege ya Shirika la Ethiopia (Ethiopian Airlines). Dk Aceng alisema mtu huyo ni mkazi wa eneo la Kibuli Kangungulu katika mji mkuu Kampala. "Mtu huyo alisafiri kwenda Dubai Machi 17, kwa sababu za biashara. Wakati wa kusafiri kwake alikuwa mzima kiafya," alisema Dk Aceng. Aceng alisema mtu huyo kwasasa ametengwa katika Hospitali ya daraja la Entebbe. Abiria wote waliosafiri na mtu huyo wako chini ya uangalizi na hati zao za kusafiria zimeshikiliwa na Serikali. Siku ya Jumamosi, Rais Yoweri Museveni alitangaza kwamba Uganda imefunga mipaka yote ili kuzuia watu kuvuka nchini kwa lengo la kujilinda na ugonjwa huo ambalo limekuwa janga duniani baada ya kuripotiwa vifo zaidi ya 10,000. Museveni leo Machi 22, 2020 atazungumza kuhusu hatua zitak...

Harmonize Aanza Kupasua Anga Kumkalisha Diamond Platnumz Kupitia Afroeast

Image
NancyTheDreamtz  Wanapotajwa wasanii wakubwa wa Bongo Fleva nchi hii, jina la Harmonize haliwezi kuwekwa kando, licha ya kuingia katika tasnia hiyo miaka michache iliyopita. Ni kama vile ameanza kupasua anga kivyake vyake nchi ya WCB, wiki iliyopita alidhihirishia hadhira kuwa ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya, kwa kufanya uzinduzi wa kishindo wa albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Afroeast2020 yenye nyimbo 18 uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Harmonize anasema licha ya kutumia muda mwingi kubuni namna atakavyofanya uzinduzi huo, alichokuja nacho kilikubaliwa na wengi ikiwamo wasanii wenzake. “Lakini nimejifunza kitu, kuwa napaswa niendelee kuwa mbunifu ili nieleweke na mashabiki wangu na wanaofuatilia muziki wa kizazi kipya. “Muziki wenyewe kwa ujumla umekuwa sana, si ajabu kukuta wimbo wa Bongofleva unasikilizwa Marekani na kwingineko duniani, hivyo kuna kitu tunafanya kinachotakiwa kuongezwa v...