MTANGAZAJI wa runinga na msanii, Mwemba Burton, maarufu kwa jina la Mwijaku, leo Jumatatu, Agosti 3, 2020, ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Dar es Salaam baada ya kusota mahabusu kwa siku kadhaa. Julai 29, 2020 mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka ya kusambaza picha za utupu ambapo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kutoka Bongo Movie au tasnia ya muziki wenye barua zilizothibitishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), ambao watasaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja. Hatimaye, dhamana hiyo ameipata leo baada ya mtangazaji wa Clouds TV na Clouds FM, Soud Brown na Charles Mwendo, kumdhamini mshtakiwa huyo. Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, ambapo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar es Salaam alisambaza picha za utupu kupitia mfumo wa WhatsApp ambapo ni kinyume na sheria. Hakimu Kabate ameahirisha kesi hiyo hadi Agos