Posts

Showing posts from November 5, 2019

Aussems: Hakuna wa kuzuia ubingwa Simba

NancyTheDreamtz K OCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amefunguka kuwa ana uhakika mkubwa wa timu yake kuweza kutetea ubingwa wake msimu huu licha ya kupoteza mchezo uliopita kutokana na ubora wa kikosi chao. Simba bado inaongoza ligi ikiwa na pointi 18 kabla ya mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Mbeya City na nyuma ya Kagera Sugar wenyewe pointi 16, wakati wapinzani wao wakubwa Azam wakiwa kwenye nafasi ya 13 wakiwa na pointi tisa huku Yanga wakiwa na pointi saba kwenye nafasi ya 17. Akizungumza na  Championi Jumatatu,  Aussems amefunguka kuwa bado wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa msimu huu na hakuna ambacho kitaweza kuwazuia kutokana na kasi ya wapinzani wao huku akiamini ubora wa timu yake kubadilika baada ya kufungwa na Mwadui wiki iliyopita. “Haikuwa mipango yetu kupoteza lakini wachezaji na benchi la ufundi tumegundua makosa yetu ambayo yamesababisha kutuondoa kwenye njia ingawa haijaweza kuharibu malengo ambayo tupo nayo kwenye ligi, maana ukiangalia

Diamond Platnumz Youngest Son’s Name Finally Revealed

Image
NancyTheDreamtz Diamond Platnumz youngest son’s name finally revealed Diamond Platnumz and his mum have finally gone ahead to reveal the name of the youngest Simba in their home. Judging from a post shared by Mama Dangote, we understand that Diamond Platnumz youngest son has been named after his daddy, Naseeb Junior. This comes as a big surprise since Hamisa Mobetto’s son had already been named after Diamond Platnumz but it appears that Mama Dangote was not satisfied by this hence the two Naseeb’s. Tanasha’s son So far many of their fans continue to wait for the 40 day celebrations that will be going down in a few days as promised by the WCB boss. Just like Latiffa Dangote, Naseeb Junior will be unveiled by his celebrity parents on his 40th day on earth and from the look of things people can’t wait to finally see him for the first time.

Yanga Yaanza na Straika Aliyeibeba Stars

Image
NancyTheDreamtz ZIKIWA zimebakia siku chache kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, uongozi wa Yanga tayari umeanza harakati zake za kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya kuhakikisha msimu huu timu hiyo inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Uongozi huo unaiangalia zaidi safu yake ya ushambuliaji ambayo tangu kuanza kwa msimu huu haijafanya vizuri kama mashabiki wengi wa timu hiyo walivyotarajia kutokana na utitiri wa washambuliaji wa kimataifa waliojiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumatatu limezipata, zimedai kuwa uongozi huo hivi sasa upo katika mazungumzo na mshambuliaji wa kutumainiwa wa Azam FC anayeichezea Polisi Tanzania kwa mkopo. Mchezaji huyo si mwingine bali ni Ditram Nchimbi ambaye hivi karibuni alifanikiwa kuipiga Yanga hat trick katika mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa Uhuru. Lakini pia kama haitoshi, Nchimbi alifanya kweli alipokuwa na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ huko nchini Sudan ambapo ali