CHADEMA Kulipa Fidia Wananchi Waliobomolewa Nyumba zao
NancyTheDreamtz Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (CHADEMA) amewataka wananchi wa Ubungo kuhifadhi vyema nyaraka zao za maeneo waliyobomolewa na kwamba CHADEMA ikiingia madarakani watahakikisha wanawalipa fidia zao. Kubenea ameyasema hayo jana ikiwa ni siku moja kupita tangu Rais John Pombe Magufuli alipotamka hadharani kuwa wahanga waliobomolewa nyumba kuanzia maeneo ya Ubungo hawatalipwa fidia kwa kuwa walivunja sheria kwa kujenga kwenye hifadhi ya barabara. Akizungumza jana na wanahabari, Kubenea amedai kushangazwa na kauli ya rais kwamba waliovunjiwa nyumba walijenga kwenye hifadhi ya barabara lakini serikali ndiyo iliyokuwa ikipokea kodi zao, kuwapatia hati za maeneo, kuwawekea maji na umeme huku wakijua hilo ni eneo la hifadhi. "Naomba wananchi wa Ubungo, Kimara waliovunjiwa nyumba zao wahifadhi vizuri nyaraka zao. Mungu akipenda Sisi CHADEMA tukiingia madarakani tutalipa waathirika wote waliobomolewa kuanzia ubungo hadi Kibaha. Inawezekana siyo...