Eymael Aigomea Adhabu ya TFF, Asema Aipo Kisheria



ALIYEKUWA kocha mkuu wa klabu ya soka ya Yanga, Luc Eymael amesema kuwa hakubaliani na adhabu iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kumfungia miaka miwili na kumtaka alipe faini ya Shilingi Milioni 8 kutokana na adhabu hiyo kukiuka taratibu za kisheria ikiwamo kutotoa nafasi ya yeye kujitetea.


 


Eymael hivi karibuni aliingia matatani baada ya kutoa kauli zilizotafsiriwa kuwa ni za kibaguzi baada ya mchezo wao dhidi ya Lipuli.


 


Akizungumza na Championi Jumatano kutokea nchini Ubelgiji, kocha Luc alisema taarifa za kufungiwa kwake hazijafikishwa kwa taarifa rasmi.




“Kwanza niseme kuwa sijapokea taarifa yoyote rasmi kutoka kwa uongozi wa Shirikisho la soka la Tanzania (TFF), kuhusu adhabu ya kunifungia na kulipa faini, hata mimi nimekuwa nikiziona taarifa hizo kupitia mitandao.


 


“Lakini suala jingine ambalo ndilo kubwa zaidi ni kwamba adhabu hii imetolewa bila kunipa nafasi ya kujitetea kitu ambacho kisheria ilikuwa haki yangu na wakili wangu aliwasilisha maombi hayo, hivyo kwa upande wangu nadhani adhabu hii ni batili na siwezi kukubaliana nayo,” alisema Eymael.

NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais