Nape Nnauye: CCM Imevamiwa na Wasaka Tonge
NancyTheDreamtz Na Bakari Chijumba, Mtwara. Wakati sakata la Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dr.Bashiru Ally na kada wa Chama hicho, Bernard Membe likiendelea kuchukua nafasi kubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameibuka na kusema CCM imevamiwa na wasaka Tonge wenye maslahi na matumbo yao kuliko chama. Nape Nnauye ambaye ni mbuge wa Mtama, ametoa kauli hiyo baada ya kuenea kwa taarifa kuhusu madai ya kuanzishwa kwa chama kipya kitakachoitwa USAWA, ambapo Bernard Membe na Nape Nnauye wametajwa kuwa miongoni mwa watakaotimkia kwenye chama hicho kipya. Taarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa wa facebook unaofahamika kwa jina la "Sauti ya Kisonge" na kuenezwa kwenye mitandao hii leo, inadai Chama hicho kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni, kinawahusisha pia mawaziri kadhaa wa utawala uliopita, mawaziri wanne kutoka Zanzibar na mabalozi kadhaa wastaafu na waliopo nje. "Chama Kipya kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni kwa jina...