Posts

Showing posts from August 15, 2019

Nicki Minaj Amuita Rick Ross Takataka Asema " Sitaki Kumsikia Mtu Anayemtukana Mwanamke Ili Auze Album Yake"

Image
NancyTheDreamtz Swali lililoulizwa na Joe lilionekana kumkwanza mwanadada Nicki Minaj baada ya kumuuliza kwamba ni nani mkali kati ya The Game na Rick Ross? Majibu ya Minaj yalikuwa makali zaidi kwa Rozzy baada ya kusema kuwa:- “Hebu usiniletee hapa hiyo takataka, usinifanye nianze kumuongelea. Mtu yeyote anayemtukana mtoto wa Kike ili kuuza vinakala 250 vya album, usimlete kabisa mbele yangu. Hongera kwa The Game, anajua kuchana.” alizungumza Nicki. Alienda mbali zaidi na kusema; Rozay hana fadhila kwa sababu alim-diss vibaya licha ya kuwahi kumsaidia msanii wake (Meek Mill) tena mbele ya Rais Obama kipindi wana mahusiano na alikuwa ameandamwa na matatizo ya kisheria. “Nilienda kukutana na Obama, na Ross alikuwepo. Nilienda kuongea naye kuhusu masuala ya “Probation” baada ya kikao nilimuona Rozay akimtumia meseji Meek na kumuambia ‘Huyu mwanamke ni wa kumtunza sana’ Halafu leo unakuja kutoa Ki-album chako na kunitukana mimi, kalisha makalio yako manene huko” Alisema Minaj

Amber Lulu 'Mimi sio wa Kufeki Maisha..Ni Kweli Nilikuwa Sina Kodi ya Nyumba Nandy Akaokoa Jahazi'

Image
NancyTheDreamtz BAADA ya habari kutapakaa kama moto wa kifuu akikiri kuokolewa na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’ baada ya kumlipa hela shoo na kulipa kodi, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amewamaindi watu mitandaoni wanaomsema vibaya kuhusu hilo. Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Amber Lulu alisema kuwa yeye siyo wa kufeki maisha hata siku moja na ni kweli alikuwa hana kodi na hela aliyompa ilimsitiri sana mbali na kulipia kodi. “Eti utakuta mtu anasema huna aibu kusema nilikuwa sina kodi kwa kumuogopa nani sasa na kwa nini maana amenipa kazi na nimefanya akanilipa shida iko wapi na nani anaumia sasa?” alimaindi Amber Lulu.

Kardinali Pengo Ang’atuka Rasmi, Papa Francis Aridhia

Image
NancyTheDreamtz ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp  Kardinali Pengo, ameng’atuka wadhifa huo na nafasi yake imechukuliwa na Askofu Mkuu Mwandamizi, Yuda Thaddeus Ruwa’ichi, wa Jimbo kuu la  Dar es Salaam. Hivi karibuni, Askofu Pengo aliomba kupumzika nafasi hiyo ambapo Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis ameridhia ombi hilo na kumruhusu kupumzika.

Kitumbo cha Tanasha Gumzo

Image
NancyTheDreamtz GUMZO kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ni muonekano mpya wa mpenzi wa mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch baada ya kuingia studio kisha kupiga picha zikimuonesha na kitumbo chake.   Tanasha anatarajiwa kujifungua wakati wowote kuanzia sasa ambapo inaelezwa kuwa, sasa hivi ujauzito wake una miezi ipatayo nane na imembadili muonekano wake huku akipenda sana kulianika tumbo hilo. Akizungumza na Amani, rafiki wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, mara ya mwisho kumuona laivu Tanasha alimshuhudia akiwa na tumbo kubwa na mara kwa mara alikuwa akijipiga picha za ukumbusho. “Mimi nimemuona, kwa kweli mimba imemkubali na vile anavyojipenda sasa ndiyo amezidi kuwa ‘mtamu’, lakini anaonekana kuwa na kaugonjwa ka’ kujipiga picha. Kila wakati atapozi na kukuomba umpige picha huku akiweka mapozi tofauti,” alisema mtoa habari huyo. Katika kudhihirisha kuwa Tanasha amekuwa na kaugonjwa ka’ picha, mwanadada huy

“Tupeni Huo Ujanja Nyie Mnafanyaje Mmefanikiwa” Magufuli kwa Ramaphosa

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuomba Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Matamela Cyril Ramaphosa kuwahamasisha zaidi wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuja kuwekeza hapa nchini kwa kuwa Tanzania inayo dhamira ya dhati ya kuongeza ushirikiano wake na nchi hiyo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Rais Magufuli amesema katika kutekeleza mipango yake ya maendeleo na dira ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 Tanzania inawakaribisha wawekezaji mbalimbali, kwa kuwa Afrika Kusini imepiga hatua kubwa katika viwanda amewaalika wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo dawa na vifaa tiba, kuchakata madini na kwamba Serikali itatoa ushirikiano wowote utakaohitajika. Rais Magufuli pia amemuomba Rais Ramaphosa kuongeza ushirikiano na Tanzania katika utalii, hasa ikizingatiwa nchi hiyo inapokea watalii zaidi ya Milioni 10 kwa mwaka ikilinganishwa na Watalii Milioni 1.5 wanaoingia hapa n