MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu wa 2020, Dkt. John Pombe Magufuli atachukua Fomu ya Kugombea Urais wiki hii katika ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma. Hayo yamesemwa leo Jumatano, Agosti 5, 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM (OND) Lumumba Jijini Dar es Salaam. “NEC imetutangazia kuanzia leo tunaweza kuchukua fomu kwa ajili ya wagombea wa nafasi ya urais. Mwenyekiti wetu na Rais wetu ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama chetu, Dkt. John Magufuli atachukua fomu wiki hii NEC, Dodoma akiomba dhamana ili akafanye makubwa zaidi kwenye muhula wa pili. Nitawaambia ni siku gani atachukua. “Kampeni tutakazozifanya mwaka huu zitakuwa ni bora zaidi na zitakuwa za kisayansi. Kwa mujibu wa tafiti tuliyoifanya mwezi Juni mwaka huu, tunaingia kwenye uchaguzi tukiwa na mtaji wa w...