Mkuranga: Aachiwa Huru Baada ya Kukiri Kumuua Mpenzi Wake


MAMLAKA ya rufaa mjini Dar es Salaam imemuondolea mashitaka mkazi wa kijiji kilichopo wilayani Mkuranga baada kukiri kuwa alimuua mpenzi wake.

Hoja ya mwendesha mashitaka ni kwamba Amani Justine aliripotiwa kumuua mwanamke aliyekua akiishi nae kama mke Gaudencia Leonce Mabuli ilijengwa kutokana na kukiri kwake kwamba alifanya uhalifu huo baada ya kudai kuwa alimpata akiwa na mwanaume mwingine kimapenzi.

Lakini Majaji walisema kuwa hoja ya mwendesha mashitaka haikuwa na ushahidi wa kuifanya mahakama iamini kuwa kulikua na uhusiano baina ya madai aliyokiri mshitakiwa na ushahidi wa mwendesha mashtaka.

Mwili wa marehemu Gaudencia ulipatikana kando ya barabara ukiwa na majeraha kwenye paji la uso, na mkononi mwezi Mei 2013. Justine aliishi na Gaudencia kwa karibu miaka mitatu, na watu wengi waliamini kuwa wawili hao ni mke na mume.

Akitoa hoja yake katika kesi ya rufaa mshitakiwa alidai kwamba Jaji wa Mahakama Kuu alikosea kumtia hatiani bila kuzingatia alivyojitetea kwamba alichokozwa, na kwamba ushahidi wa mwendeshamashitaka haukuthibitishwa.



NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele