Posts

Showing posts from August 2, 2020

Nafasi za Kazi Global Group; Marketing Dept na Global TV

Image
NancyTheDreamtz

Dj Cuppy Amkubali Rayvanny!

Image
M KALI  wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny, ameendelea kupaa kimataifa baada ya kukubalika kinoma na DJ mrembo kutoka Nigeria, DJ Cuppy kumshirikisha kwenye Ngoma, Jollof On The Jet na staa mwingine wa nchini humo, Rema. DJ Cuppy ameweka wazi kuwa katika ngoma hiyo iliyotoka juzikati ina mchanganyiko wa ladha za Afro- Pop na Afro-Beat huku Rayvanny na Rema ambao wote ni washindi wa tuzo za BET wakionesha uwezo mkubwa. “Kufanya kazi kwa ushirikiano huu wa Rayvanny na Rema wa hapa Nigeria umenitia moyo, hii ni Afro-Pop iliyoboreshwa, japo hatujarekodi pamoja studio, lakini tumetoa ngoma kali ambayo naamini kila mmoja ataipenda hivyo naomba sapoto kutoka kwa mashabiki Afrika Mashariki,” amesema DJ Cuppy ambaye tayari amefanya kazi na mastaa kibao akiwamo Tekno na Zlatan. DJ Cuppy alianza kujipatia umaarufu mwaka 2014 kwenye Tuzo za MTV Africa Music na mwaka uliofuata alifanya ziara yake ya Cuppy Takes Africa Tour ambayo iliwekwa kwenye makala ya Fox Life. NancyTheDreamtz

Nina Ugonjwa wa Kuiba Chupi za Wanawake..Nifanyaje Niache?

Image
Kila nikilala na mwanamke kama kabeba chupi ya kubadili ile aliyovaa akiivua lazima nifanye manuva mpaka niondoke nayo, alafu nazitumia baadae kuvuta hisia kwenye mambo yetu ya kisabuni.. Sasa uvungu wangu chumbani umejaa chupi na nyingine zinanuka kweli... Nafanyaje niweze kuacha hii tabia? NancyTheDreamtz

Shilole ampa makavu live Snura Mushi mbele ya umati

Image
"Kuna Wanawake tunapendana na kuna Wanawake wengine hatupendani, Dada yangu Snura Mushi aliposikia nimepigwa eti akasema apigwe tu, makavu live mimi sina siri, Mwanamke lazima umuonee huruma Mwanamke mwenzio, nakupenda Snura ndio maana nakuambia ukweli”-SHILOLE NancyTheDreamtz

Shirika la WHO laonya kuwa janga la corona litachukuwa muda mrefu

Image
Shirika la afya duniani WHO limeonya jana kuwa janga la virusi vya corona litadumu kwa muda mrefu na huenda likasababisha ''kulemewa kwa mikakati ya kukabiliana nalo'' huku India na Ufilipino zikiripoti ongezeko la maambukizi mapya. Miezi sita baada ya shirika hilo la WHO kutangaza janga hilo kuwa dharura ya kimataifa, shirika la habari la AFP limeripoti kuwa virusi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 680,000 na maambukizi ya zaidi ya watu milioni 17.5. Kamati ya dharura ya shirika hilo inayofanya tathmini mpya kuhusu janga hilo, imesema janga hilo linatarajiwa kuwa la muda mrefu na kutaja umuhimu wa kudumisha juhudi za kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa za kukabiliana na virusi hivyo.  Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, shirika hilo la WHO limesema linaendelea kukadiria kiwango cha hatari cha kimataifa cha COVID-19 kuwa juu sana. NancyTheDreamtz

Magufuli apiga simu Tamasha la Nguvu ya Mwanamke

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Tamasha la Nguvu ya Mwanamke (Girl Power), linatakiwa liwe endelevu ili liweze kusaidia kujua vipaji vya wasichana vinavyotakiwa kuendelezwa ili kufikia maendeleo ya taifa. Amezungumza hayo leo Agosti 2, 2020 alipopiga simu wakati Tamasha likiendelea nakuongea na wanawake waliopo katika Tamasha hilo huku akiwapongeza na kueleza ni kwa jinsi gani amefurahishwa na tamasha hilo linalolenga kumjenga mwanamke. "Nimefurahi kipindi hiki ni kizuri na kinatakiwa kiendelezwe ili kusudi tujue vipaji vya wasichana ambao tunatakiwa kuwaendeleza katika maendeleo ya taifa hili", amesema. Aidha Rais Magufuli amesema kuwa wakina mama pamoja na wakinadada wa Tamasha hilo la Nguvu ya Mwanamke wanaweza na amefurahishwa nao sana. “Ningetamani niwe hapo na nyie ila nimefurahi, tuko pamoja, siku nyingine na mie mnikaribishe tuwe pamoja, nipo pamoja nanyi, mmeninsipire sana mmefanya kazi kubwa kwa Taifa hili, Wanawake sitowaach...

Diplomasia ya Uchumi Kumbeba Magufuli Uchaguzi wa Urais Oktoba 2020

Image
Ukiacha jinsi alivyosimamia rasilimali kwa maslahi ya Watanzania namna alivyolikabili janga la COVID-19 hususani dhidi ya sera dhidi ya WHO na baadhi ya mataifa mengine. Tukija visa na mikasa ya majirani hususani Kenya, JPM ameonesha msimamo usioyumba, hakika ramani ya Tanzania imeng'aa. Hata wafuasi wa CHADEMA waliopo kwenye Jukwaa la Kenya wamebaki midomo wazi wasipate la kubwabwaja. Itoshe tu kusema Tanzania inahitaji Amiri jeshi Mkuu mwenye hulka ya JPM ili kutuvusha kwenye diplomasia ya uchumi. Tunamuhitaji Magufuli tena! NancyTheDreamtz

Mwanamitindo aeleza kuumia baada ya Vanessa Mdee kuacha muziki, Nilitamani kufanya nae kazi (+Video)

Image
Msanii na Mwanamitindo Chrispnin amefungukamengi kuhusu kazi yake ya uanamitindo na kazi yake ya uigizaji. Akiongea na Bongo5 ameeleza kuwa kazi ya Uanamitindo ni kazi ngumu sana na inayohitaji uvumilivu na kwa mara nyingine watu huwaponda na kuwaambiakuwa wanafanya kazi hiyo ili wapate wanawake kumbe sivyo bali wanafanya kwa ajili ya maisha. Ameongeza kuwa katika kazi yake ya Uanamitindo alikuwa anatamani sana kufanya kazi na Vanessa Mdee ila ameumia sana baada ya Vanessa kutangaza kuachana na muziki. “Niliumia sana Vanessa alipotangaza kuacha muziki ila naamini kuna siku ntafanya nae tu” NancyTheDreamtz

Jeuri ya pesa kati Diamond na familia ya Msizwa, ni mashindano (Video)

Image
Leo mtanange wakushindana kumtuza pesa bibi harusi kati ya Wasizwa ambao wamekuoa @_esmaplatnumz pamoja na @diamondplatnumz .   Mchuano ulikuwa mkali sana kati ya familia hizo mbili ingawa kulikuwa na changamoto za kubishana. Hebu angalia mtanange halafu utoe maksi zako. NancyTheDreamtz

Kamati kuu ya CHADEMA kutoa mapendekezo yao leo, juu ya mgombea Urais kabla ya kuwasilishwa baraza kuu kesho

Leo Agosti 2, 2020 Kamati kuu ya CHADEMA inakaa kikao ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kutoa mapendekezo yao kutokana na utafiti waliofanya wa wagombea kwa upande wa Urais wa Tanzania Bara na Zanzibar na kuyawasilisha katika kikao cha Baraza kuu kitakachofanyika kesho. NancyTheDreamtz

Aubameyang kujiunga na Chelsea, mashabiki washtushwa na taarifa hizo

Image
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ameshangaza watu baada ya kuibuka kwa taarifa za kuwa anafikiria kuhamia Chelsea mwezi Januari. Aubameyang mwenye umri wa miaka 31, ameonyesha nia hiyo ya kuhamia The Blues siku moja kabla ya mchezo wao wa Fainali kombe la FA Cup. Hata hivyo hadhima yake ya kuhamia Chelsea imeonekana kugonga mwamba baada ya Chelsea kutokuwa na kiasi kikubwa cha fedha cha kumlipa Aubameyang. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao, Aubamayeng amesajiliwa Arsenal akitokea Borussia Dortmund kwa dau la paundi milioni 56 mwaka 2018. Kocha wa Chelsea, Frank Lampard kwa sasa anatafuta mchezaji wa safu ya ushambuliaji lakini hana msuli wa kumlipa nyota huyo raia wa Gabon na kama atahitaji kuitumia The Blues lazima Aubamayeng ashushe dau lake la mshahara. Aubameyang amefunga jumla ya magoli 27 msimu huku Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta akifanya kila jitihada kuhakikisha anambakiza nyota huyo ambaye pia anawindwa na Barcelona na AC Mi...

Mnyama Simba alichukua na kombe la Azam Sports ASFC, aandika rekodi hii

Image
Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Mnyama Simba amefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports ASFC 2019/20. Simba sasa inaandika historia kwa kuwa timu ya kwanza kuchukua kombe hili la Azam Sports ASFC zaidi ya mara moja. Mnyama ameunguruma katika nyasi za Nelson Mandela Stadium kupitia kwa wachezaji wake Luis Jose Miquissone dakika ya 27’ na Nahodha John Bocco dakika ya 39’ ya mchezo. Namungo wamejaribu kuchezea ndevu za Mnyama dakika ya 57′ kupitia kwa Edward Charles lakini hata hivyo walishindwa kufua dafu mbele Simba na mpira kumalizika kwa goli 2 – 1.   Related Articles NancyTheDreamtz

Rais Magufuli apokea hati za utambulisho wa Mabalozi

Image
Rais Dkt. John Magufuli leo tarehe 02 Agosti 2020 amepokea hati za utambulisho wa Mabalozi wa wawili. 1.Mhe. Nguyen Nam Tien Balozi Mteule wa  Vietnam  Nchini Tanzania 2.Mhe. Donald John Wright Balozi Mteule wa  Marekani  hapa Nchini.   NancyTheDreamtz