MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amefunguka kuhusu taarifa zinazodai yuko mbioni kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tangu mwaka jana, wimbi la viongozi, wabunge na madiwani wa upinzani kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM lilipoanza, Kubenea amekuwa akihusishwa na mpango wa kuihama Chadema na kujiunga na chama tawala. Juzi aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akitetea uamuzi wa viongozi wa upinzani kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM. Ujumbe huo wa mbunge huyo anayefahamika kwa kutoa habari nyingi za msingi wa makatazo na machukio dhidi ya watu walio mafisadi nchini akiwa mwandishi wa habari, ulisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuibua mjadala kutokana na kuhusishwa kwake kwa muda mrefu kujiunga na chama tawala. Ujumbe huo ulisomeka: "Si wote wanaohama wamenunuliwa, ingawa ni kweli kuwa wapo baadhi ya waliohama wamenunuliwa. Kuna wengine wamehama kutokana na kuwapo migogoro, chuki na ubaguzi katika maeneo