Posts

Showing posts from August 6, 2019

LIVE SIMBA DAY: HALI ILIVYO UWANJANI TAIFA MUDA HUU

Image
NancyTheDreamtz

LIVE SIMBA DAY: HALI ILIVYO UWANJANI TAIFA MUDA HUU

Image
NancyTheDreamtz

Mwanamke Kaamua Kufunga Ndoa na Mbwa Baada ya Kutembea na Wanaume 221

Image
NancyTheDreamtz Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Elizabeth Hoad raia wa Uingereza,  amefunga ndoa na Mbwa wake aitwaye Logan katika kipindi cha Television Nchini humo. Baada ya kufunga ndoa, Mwanamke huyo ameeleza aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Wanaume 221, kati ya hao Wanne ndio walimvalisha pete ya uchumba lakini imeshindikana kuolewa. Pia mwanamke huyo amesema ameamua kufunga ndoa na Mbwa wake "Logan", kwa sababu ya kuchoshwa na Tabia za Wanaume wazee kupenda Wanawake wadogo na Wanawake wadogo kupenda Wanaume wazee. Aidha Elizabeth ameendelea kusema Mbwa huyo ana maana kubwa sana kwake kwa sababu wameshasaidiana kwa vitu vingi hasa wakati alipoumizwa na Wanaume ambao aliwahi kuwa nao, pia ana marafiki zake 10 ambao wameamua kufunga ndoa na Mbwa wao. Akiweka kiapo katika sherehe ya kufunga ndoa hiyo Elizabeth aliahidi kuwa, "kwa mwili wake wote atatembea na Mbwa Logan, atamjali na kumpenda siku zote za maisha yake na kulala nae kitanda kimoja" amese...

Wakazi wa Mtwara Watakiwa Kuongeza Kasi ya Uzalishaji wa Mazao

Image
NancyTheDreamtz Wakazi wa mkoa wa Mtwara wametakiwa kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili waweze kutumia vizuri fursa za ujenzi wa miundombinu ya barabara, anga na bandari kujiimarisha kiuchumi. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi),Elius John Kwandikwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ukanda wa kusini mwa Tanzania unafunguka kimiundombinu katika nyanja za barabara za lami, bandari na usafiri wa anga hivyo kazi inayowakabili wananchi ni kuongeza uzalishaji. Akizungumza na wanakijiji wa Nanguruwe mkoani humo, Kwandikwa amesisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuweka fursa ya miundombinu bora katika kila kanda ili wananchi waitumie kukuza uchumi binafsi na hivyo kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025. “Tumejipanga kuhakikisha nyanja zote za usafiri zinaimarika katika ukanda huu wa kusini hivyo nawaomba zalisheni kwa wingi mazao ya chakula na biashara ili kufikia soko kwa haraka popote lilipo,” amesema Kwan...

Simba Yatangaza Usajili wa Mchezaji Mwingine

Image
NancyTheDreamtz Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake Haji Manara ameweka wazi kuwa, leo watamtangaza mchezaji mmoja ambaye mpaka sasa alikuwa hajaungana na kikosi kwenye maandalizi ya msimu ujao. Akiongea kwenye 5SPORTS ya East Africa Television, Manara ameeleza kuwa kuna 'suprise' watu wajiandae kumjua kesho wakati akimtambulisha. ''Kuna mchezaji mpya kabisa na anacheza nafasi zote uwanjani, nitamtambulisha wa mwisho'', alisema Manara. Manara pia ameongeza kuwa, tayari kocha Patrick Aussems ameshapewa malengo ya msimu ujao wa 2019/20, ambapo anatakiwa kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa ligi kuu kisha kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba leo wanaadhimisha tamasha lao la 'Simba Day' ambapo linafanyika kwa mara ya 10 mfululizo ikiwa ni maalum kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kutambulisha wachezaji watakaowatumia msimu mzima.