Posts

Showing posts from October 3, 2018

Zari Achafua Hali ya Hewa Instagram......Ni Baada Ya Kumwandikia Diamond Ujumbe wa Dharau na Kuwaita Wanae KIMA

Image
NancyTheDreamtz Leo ni siku ya kuzaliwa kwa muimbaji Diamond Platnumz, watu wake wa karibu, ndugu, marafiki na mashabiki wamekuwa wakimtumia salamu za kheri kwenye siku yake hiyo muhimu. Ujumbe wa Zari The Bosslady ulikuwa ukisubiriwa sana mara baada ya Diamond kumuandika ujumbe mzuri sana mrembo huyo siku kadhaa zilizopita kwenye Birthday licha ya kuachana kwao. Sasa Zari The Bosslady ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha ya watoto wake na Diamond kisha kuandika ujumbe wa dharau;  'Happy birthday mwenye vikima vyake'. Kwa ujumbe huo, watu wengi wamesikitishwa na kitendo cha mwanamama huyo kuwafananisha watoto wa Diamond Platnumz na mnyama KIMA. 

Video Mpya ya Mr Nice: Tuvumiliane

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa Bongo Fleva, Mr. Nice anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya uitwao Tuvumiliane. Itazame hapa. Advertisement

Diamond kuwasaidia watoto 300, kina mama 200 Tandale ....Pia Kaahidi Pikpiki 20 Kwa Vijana wa Tandale

Image
NancyTheDreamtz Katika kusherekea siku yake ya kuzaliwa msanii Diamond Platnumz ameamua kufanya kitu cha kipekee zaidi. Muimbaji huyo ambaye Birthday yake ilikuwa hapo jana, October 02, 2018 amepanga siku ya Ijumaa wiki hii kufanya tukio la kutoa misaada Tandale ambako ndipo amezaliwa. "Jambo la kwanza kabisa ni kuzungumza na vijana wenzangu wa Tandale na kuwapa maneno fulani ya kuwaongezea moyo. Siku hiyo nitatoa bima ya afya kwa watoto sio chini ya 300," amesema. "Vile vile tutakuwa tunatoa mitaji kwa wamama wasiopungua 200 wa pale Tandale kwa hiyo birthday yangu nitakuwa naisherekea hivyo," Diamond ameiambia Wasafi TV. Pia Diamond ameongeza kuwa atatoa bodaboda 20 kwa vijana ambao hawana ajira pamoja na kukarabati baadhi ya shule hapo Tandale.

Mzee Mwinyi: Rais Magufuli Mimi Nina Kuhusudu Kwasababu Unafanya Mambo Mazuri Kwa Wananchi

Image
NancyTheDreamtz Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi hii leo October 2 alikuwa mmoja wa waalikwa kwenye Ikulu ya Rais Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje sambamba na kuapishwa kwa mkuu wa Skauti nchini.  Mlezi huyo wa Skauti nchini Alhaj Ali Hassan Mwinyi akapewa nafasi ya kutoa neno kwa rais Magufuli. Katita salamu zake fupi, Rais Mstaafu Mwinyi amesema kuwa aliomba kustaafu kuwa Mdhamini wa Skauti Tanzania ombi ambalo lilikataliwa na Rais Magufuli,na kusema kuwa bado vijana wana mambo mengi ya kujifunza kutoka kwake. Pia Mzee Mwinyi amesema anamhusudu  sana Rais John Magufuli kwa sababu anafanya mambo mazuri kwa wananchi wa Tanzania  na yanamgusa sana. ==>>Naomba nisimalize utamu wote, Mzekilize Mzee Mwinyi hapo chini

Nilikataa Wema Asifanye video na ROSTAM :-Mke wa Roma

Image
NancyTheDreamtz Mke wa msanii Roma  anaejulikana sana kwa jina la Mama Ivan amefunguka na kusema kuwa alikataa wazo la wasanii hao kutaka kutoa video yao ya wimbo mpya unaojulikana kama ameolewa kwa kumtumiaWema Kama video queen katika wimbo huo. Mama Ivan mabe siku ya jana alifika katika mjengo wa Clouds Media kwa ajili ya kwenda kutambulisha wimbo mpya wa mume wake akiwa pamoja na mke mwenzake  mke wa stamina anasema kuwa kufanya hivyo haikuwa kwa ubaya. Mama Ivan anasema kuwa wakati mume wake wanabisha na kuhusu mwanamke gani wa kumtumia katika video hiyo, wenyewe waliamua kuwa awe Wema lakini yaya alikataa kutokana na uhalisia wa wimbo kwamba inabidi mwanamke aendane na uhalisia na kuona kuwa Wema asingeweza kukaa katika nafasi hiyo. Mke wa Roma  na Stamina wamevunja rekodi ya kwanza kwa wasanii kuonyesha kuwa hata familia zao zimekuwa zikisapoti kazi zao, kwa sababu tumekuwa tukiona wasanii wanasaidia wenyewe kwa wenyeke katika utambulisho wa nyimbo lakini ROSTAM...

Tunda Abambwa na Diamond Baada Ya Kumwaga Casto

Image
NancyTheDreamtz Socialite na video queen maarufu Bongo Tunda Sebastian amerudi Kwenye headlines baada ya kuonekana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz. Tunda ameshawahi kusemekana kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond lakini baadae alianzisha Mahusiano na Mtangazaji wa clouds Tv Casto Dickson. Pamoja na kwamba Casto alichora bonge la Tattoo ya Jina la Tunda Kwenye Mkono wake lakini aliishia  wiki chache zilizopita na siku ya jana ameonekana Kwenye Birthday party Diamond. Diamond alionekana akicheza na Tunda kwa ukaribu sana kiasi ya kupelekea kuzua tetesi za kuwa Tunda kamtosa Casto na Kurudisha majeshi yake kwa Diamond.

Klabu ya Simba Yampa Tuzo Maalumu Diaamond Platinum Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Image
NancyTheDreamtz Afisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara hapo jana amemkabidhi tuzo msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz kwa niaba ya klabu hiyo. Manara amemkabidhi Diamond tuzo hiyo kwenye siku yake ya kuzaliwa hapo jana siku ya Jumanne mbali na zawadi hiyo amempatia keki yenye nembo ya Simba kutokana na msanii huyo kuwa shabiki mkubwa wa klabu hiyo. Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Manara amemwagia sifa msanii huyo kuwa ni mwanamuziki mkubwa ulimwenguni. Branding ya kitu chochote kile haijengwi kwa kukaa ofisini peke yake na mifaili na milaptop kama ww ndio uliyeanzisha Microsoft..ni kutoka ktk events na matukio tofauti..maana ya media officer wa club ni zaidi ya publicity secretary..halaf Simba ikiongoza kwa mapato mtatafuta mchawi.. hv mnajua kwa Jay Zee na Rihana kujitangaza tu ufuasi wao kwa Arsenal nn walipata wajukuu wa Babu Wenger? Unadhani mm mjinga kutumia ushawishi wa kina. Kwa kadri ilivyo ww ni Msanii na Mwanamuziki mkubwa c Bongo tu bali kote Uli...

MUSIC VIDEO: Belle 9 – Take Away

Image
NancyTheDreamtz Belle 9 kwa mara nyingine amedondosha kichupa cha ngoma yake mpya ya Take Away, mdundo wa ngoma hii umetengenezwa na Mr T Touch na video imeongozwa na Digital Vibes & Lion Head. Enjoy!

Video: Major Lazer ft Burna Boy – All My Life

Image
NancyTheDreamtz Major Lazer kutoka Marekani, wamechia video ya wimbo wao mpya uitwao ‘All My Life’ huku wakiwa waememshirikisha msanii wa Nigeria, Burna Boy.

Alikiba aachia video ya wimbo Hela, agusia rushwa hospitalini na wanyonge kunyimwa haki

Image
NancyTheDreamtz Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye Alikiba Jumatano hii ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Hela’. Muimbaji huyo amezungumzia namna pesa inavyowatesa watu mbalimbali katika kupata mahitaji yao muhimu huku akitolea mfano watu wanavyokosa huduma hospitali kisa hela.

Diamond aonyesha mjengo wake mpya siku ya birthday yake ( VIDEO)

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki wa kizazi kipya na C.E.O wa WCB Wasafi Diamond Platnumz ameweza kuonyesha nyumba yake mpya jioni ya leo ikiwa ni siku ake ya kuzaliwa. Msanii alikuwa kwenye show yake nchini Zambia hivyo baada ya kurejea ameweza kutumia akauti yake ya instagram kupitia insta stori kutuonyesha nyumba yake mpya akiwa na wasanii wenzake wa WCB. Hii inaelezwa kuwa ni majibu kwa aliyekuwa mwanamke wake Zari baada ya kuposti ujumbe uliozua gumzo akiwa anamtakiwa kheri katika siku yake ya kuzaliwa,kwa kupost picha inayoonyesha watoto wake wawili Tiffa pamoja na nillan huku akiandika ” happy birthday mwenye vikima vyake” Hivyo wengi wandai kuwa hayo ndio majibu ya diamond kwa mama watoto wake wa zamani Zari.