Zari Ammisi Diamond Platnumz
B AADA ya kuachana na bwana’ke mwingine aliyepewa jina la Dark Stallion (Farasi Mweusi), baby mama wa staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz, Zarinah Hassan au Zari The Boss Lady amesababisha sintofahamu, IJUMAA limedokezwa. Mwanamama Zari ambaye ni raia wa Uganda mwenye maskani yake, Durban nchini Afrika Kusini, amesababisha mjadala mpya kutoka kwa wafuasi wake almaarufu Team Zari kwamba ni rasmi sasa amerejesha majeshi kwa mwamba Diamond. ZARI AMEMMISI MONDI? Team Zari wanadai kwamba, Zari amesababisha mshangao kwao baada ya kudaiwa kummisi Diamond au Mondi; muda mfupi baada ya kumwagana na huyo Dark Stallion ambaye jina lake halisi ni Frederick Nuamah, mwigizaji na prodyuza mkubwa wa filamu nchini Ghana. Zari ambaye ni mama wa watoto watano, anasema kuwa, anammisi mtu f’lani ambaye Team ...