Kwa Ishu ya King Bae Unajitekenya na Kucheka Mwenyewe!
NancyTheDreamtz Z ARINAH Hassan ‘The Boss Lady’ ni miongoni mwa wanamama maarufu Afrika Mashariki ambaye kwa namna moja au nyingine, umaarufu wake umekua zaidi baada ya kukutana na kuzaa watoto na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Wakati penzi lake na Diamond au Mondi linachipukia, watu wengi hususan Wabongo walikuwa hawamjui kivile. Baada ya kuanza uhusiano na Mondi ndipo watu sasa wakaanza kumfuatilia na kujua shughuli zake licha ya kuwa kwenye uhusiano huo bado kulikuwa na maswali mengi yaliyokosa majibu kwa mrembo huyo. Watu walikuwa wakihoji kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii anajinasibu na magari mengi ya kifahari yenye namba zilizosomeka Zari1, Zari2 na mengine kibao, je, yalikuwa ni ya kwake kweli kwa maana ya kumiliki au la? Achana na hilo, kuna lile suala la shule na maduka anayodaiwa kumiliki nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ bado na vyenyewe vilikuwa ni kitendawili. Hakuna aliyeweza kutegua moja kwa moja kama ni kweli anamilik...