Posts

Showing posts from September 9, 2020

Mserbia Yanga SC Ampa Shavu Carlinhos

Image
KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi kuu. Carlinhos ambaye amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1. Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti. “Carlinhos ni mchezaji mzuri, tunatarajia kupata ufundi wake hivi karibuni lakini kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa kuwa bado hana utimamu wa mwili katika kucheza mechi ila hivi karibuni ataonekana uwanjani. “Ukiachana na yeye pia bado kuna wachezaji wengi ambao hawajawa fiti lakini tunatarajia kupata ubora wao huko mbeleni kwa kuwa wanahitaji muda kuonyesha ubora wao,” alisema kocha huyo. Yanga inatarajia kumenyana na Mbeya City katika mchezo ...

Mastaa Hawa Wamefunikana Kwelikweli Kwenye Ligi

Image
TAYARI kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kimeanza ambapo timu nyingi kwa sasa zimeanza kusaka pointi tatu ndani ya uwanja kwa msimu wa 2020/21. Mabingwa watetezi ni Simba, walitwaa taji hilo msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kujiwekea kibindoni pointi 88. Tayari Septemba 6 walikiwasha huku na watani zao wa jadi Yanga nao walikiwasha pia.Simba wao walikuwa Uwanja wa Sokoine kumenyana na Ihefu ambapo ilishinda mabao 2-1, Yanga wao walijiwekea ngome pale Uwanja wa Mkapa na ilitoshana nguvu kwa safari yake imeanza ndani ya Uwanja wa Sokoine na ana kazi ya kukiongoza kikosi chake kutetea taji la Ligi Kuu Bara. Bocco aliyeyusha dakika zote 90 na alikiri kwamba Ihefu FC sio timu ya mchezomchezo ndani ya ligi licha ya kwamba ni msimu wake wa kwanza. JOASH ONYANGO Licha ya kwamba hakuwa na chaguo wakati akishuhudia shuti la Omary Mponda likizama ndani ya nyavu za kipa wake Aishi Manula, Onyango alipambana. Kazi kubwa ilikuwa ni kuokoa hatari za Jordan John ambaye alikuwa ni msumbuf...