Posts

Showing posts from October 14, 2018

KUMBUKIZI ZA MWALIMU NYERERE WALIVYO ZIAZIMISHA WILAYA YA NANYUMBU LEO MANGAKA 14/10/2018

Image
NancyTheDreamtz Viongozi wa Wilaya ya Nanyumbu Leo  Wilayani Nanyumbu Mkoa wa Mtwara hawakuwa nyuma kuhakikisha kwamba wanamuenzi BABA WA TAIFA kwa Heshima na Taadhima kwa Weledi mkubwa aliowahi kufanya MWALIMU  Nyerere Viongozi wa Vyama vya Kisiasa bilakujali utofauti wa Vyama walihudhuria na kushiri Mdahalo kwa kuelezea mambo mbalimbali ambayo Kiongozi wetu Mwalimu ameweza kuyafanya katika harakati za kutafuta ukombozi kwa nguvu kubwa pamoja na kuimarisha Umoja na mshikamo katika kulifanikisha hilo Baba wa Taifa letu aliweza kushirikiana na akina Mzee Kingunge,Bibi Titi Mohamed na wengine wengi sana ambao kwaujumla wao waliweza kuimarisha Taifa la Tanzania kupiga hatua za Kisiasa,Kiuchumi na Kijamii katika Taifa la Tanzania hadi kuwa Tanganyika.  Akiongea katika Mdahalo huo Katibu wa CCM Wilaya ya Nanyumbu Ndugu Paul Mwita aliweza kumuelezea Mwalimu kwa Mapana zaidi .        

Nyerere Day: Rais Magufuli na Mkewe Wamtembelea Mama Maria Nyererer Nyumbani Kwake

Image
NancyTheDreamtz Leo tarehe 14 mwezi wa 10 Taifa la Tanzania linaadhimisha kumbukumbuku ya miaka 19 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo Rais John Magufuli na mkewe, Mama Janeth Jumapili hii wamekwenda kumtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema, Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Julius Nyerere kwa kuhakiksha fikra na mipango mizuri aliyoiweka inatekelezwa kwa manufaa ya Watanzania wote. Amesema, Baba wa Taifa alifanya kazi kubwa kujenga misingi imara ya nchi kuwa na amani, umoja na mshikamano na pia kujenga misingi ya uchumi wa kujitegemea kupitia Azimio la Arusha. Akiwa nyumbani kwa Mjane wa Baba wa Taifa, Rais Magufuli pia alikutana na mtoto wa Mwl. Nyerere, Makongoro na wajukuu wa Baba wa Taifa. Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo n

Hofu ya kuhamia CCM inavyomtesa Kubenea, Atumia Nguvu Nyingi Kujibu

Image
NancyTheDreamtz Vuguvugu la wabunge wa vyama vya upinzani kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuunga mkono jitihada za Rais, Dkt John Pombe Magufuli bado linaendelea ambapo mpaka sasa jumla ya wabunge nane wameshakumbwa na vuguvugu hilo. Www.eatv.tv imefuatilia baadhi ya matamko na maandiko ya Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea juu ya nguvu kubwa anayoitumia kukanusha madai ya kuwa huenda akatangaza kukihama chama chake cha CHADEMA muda wowote, hali ambayo ni tofauti kwa baadhi ya wabunge wengine wanaotajwa. Hivi karibuni kupitia baadhi ya vyombo vya habari ilitajwa orodha ya majina ya wabunge 15 wenye hatihati ya kuhama vyama vyao akiwemo, Mbunge Ester Bulaya, John Mnyika, aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe Joseph Mkundi ambaye nae amehama CCM na Saed Kubenea ambaye yeye ameonekana kuzua sintofahamu mpaka sasa kutokana na nguvu anayoitumia kujibu madai hayo. Disemba 2017, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kubenea alikanusha taarifa za kutaka kuhamia CCM kwa kil