Madee atoa neno baada ya Mr Blue kuanguka jukwaani



Kufuatia tukio la Mr Blue kudondoka jukwaani kwenye tamasha alilofanya weekend iliyopita, msanii Madee Ali ametoa wazo kwa wasanii wengine kukata bima za maisha na afya zao na sio kukimbilia kukata bima za magari kwa sababu ya kuogopa kukamatwa na traffic.


Akiandika wazo hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais huyo wa Manzese Madee ameeleza kuwa, "Nimeona video Herry Samir Mr blue ameanguka jukwaani, natoa pole kwa niaba ya wanamuziki wote, Mungu akusimamie urudi tena kazini".


"Ifike muda sasa wasanii mjikatie bima za maisha yenu, msikimbilie kukatia bima magari kisa unaogopa kukamatwa na traffic, hizi ajali za majukwaani zimekua nyingi siku hizi, hela uliolipwa unaenda kujitibia ni wazo tu " ameongeza Madee.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele