Ifahamu Siku ya Ijumaa Kuu Kiundani...
NancyTheDreamtz Siku kama ya leo saa tisa alasiri, ni maarufu kama Ijumaa Kuu, katika nyumba za ibada za Kikristo, kimya hutanda, mishumaa huzimwa na kuashiria kuwa ni siku ya majonzi. Ijumaa Kuu ni siku ambayo Wakristo duniani kote hukumbuka mateso aliyoyapata Yesu Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeipa thamani siku hii kwa kuitangaza kuwa ya mapunziko. Siku hii huadhimishwa kwa ibada inayoambatana na kusoma mistari ya Biblia inayoelezea undani wa matukio yaliyosababisha kusulubiwa kwa Yesu Kristo miaka zaidi ya 2000 iliyopita. Hii ni siku ambayo inatajwa kuwa na maana kubwa katika imani ya Kikristo. Waumini wanaamini kwamba, kusulubiwa na kufa kwa Yesu, kumeleta ukombozi duniani kote. Ijumaa Kuu haithibitishwi tu na vitabu vya dini, bali hata machapisho ya kihistoria, yanathibitisha juu ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu. Huadhimishwa kwa ibada huku zikitawaliwa na mistari na nyimbo za maombolezo ya kufa kwa Yesu. Rangi za vitambaa vipamb...