Straika Mpya Yanga Aitisha Simba

MSHAMBULIAJI mpya wa kikosi cha Yanga, Waziri Junior ametamba kuwa ametua ndani ya klabu hiyo ili kumaliza utawala wa muda mrefu wa Simba na mshambuliaji wao Meddie Kagere.

 

Waziri ambaye msimu wa 2019/20 aliibuka mfungaji bora wa klabu ya Mbao baada ya kutupia mabao 13 alitambulishwa rasmi ndani ya Yanga siku ya Jumapili jioni baada ya kukamilisha usajili wake na kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Waziri ambaye anatajwa kuwa kati ya washambuliaji mahiri alisema licha ya kutambua kuwa haitakuwa kazi rahisi kufanikisha hilo lakini amejipanga na anaamini ataweza kulifanikisha.

 

“Tangu mwaka 2015, nilipoanza rasmi kucheza Ligi Kuu Bara kwenye klabu ya Toto Africans ndoto yangu ilikuwa ni kumaliza msimu nikiwa mfungaji bora, nashukuru Mungu kwa kuweza kukamilisha usajili wa kujiunga na Yanga kwani sasa ninaona dhahiri kuwa nipo karibu kukamilisha malengo hayo.

 

“Najua haitakuwa kazi rahisi kutokana na uwepo wa washambuliaji wengi bora kama, Meddie Kagere wa Simba ambaye tayari ameitwaa tuzo hiyo kwa misimu miwili mfululizo, lakini ninaamini kuwa kwa msaada wa ushirikiano wa wenzangu nitaweza kuumaliza ufalme wake na kuizima Simba kuchukua tuzo hiyo tena msimu ujao,” alisema Waziri.

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele