Posts

Showing posts from August 12, 2018

Nini ameniacha lakini bado nampenda, akitaka kurudi nipo tayari – Nay wa Mitego

Image
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego kwa mara ya kwanza amefunguka kuzungumzia namna alivyoachana na mpenzi wake ‘Nini’. Mrembo huyo ambaye pia bado anadaiwa kuwa ni msanii wa Free Nation label ya rapa huyo, alidai ameamua kumuacha rapa huyo kwa madai amekuwa na michepuko mingi.

Ben Pol adai muziki wa Bongo Fleva umeshuka kidogo, awahusisha BASATA

Image
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema kuwa kwa sasa muziki huo umeshuka kidogo na hii ni kutokana na presha kwa wasanii, vyombo na taasisi za kiserikali zinazosimamia muziki huo. Ben Pol Ben Pol amefunguka hayo kwenye mahojiano yake na EATV kwenye kipindi cha Kikaangoni ambapo amedai kuwa “ Bongo Fleva na yenyewe kama imetetereka hapa katikati, naona kama kuna presha ya kutoa muziki mzuri, kuna presha ya kuwa relevant, kuna presha ya wasanii wachanga kutoka, kuna presha ya vyombo kama taasisi kumekuwa na presha ambao ndio walezi wetu, “amesema Ben Pol na kuwazungumzia BASATA. “BASATA ni chombo na chombo pia kinaongozwa na binadmu, hata tukikataa hatuwezi kujikataa kuwa sisi ni binadamu wote sisi ni binadamu. Kunaweza kuwa na makosa ya kibinadamu pia taasisi yoyote au chombo chochote kwa sababu kinaongozwa na binadamu kinaweza kikawa na makosa ya kibinadamu. Naheshimu namna ambavyo wanasimamia na wanapigania sanaa yetu lakini sote ni binadamu. “amemaliza Ben Pol. W...

Mashabiki wamshusha Davido jukwaani nchini Namibia, wahuni wamvua saa na viatu (+video)

Image
Jana usiku msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido amejikuta akishushwa jukwaani na mashabiki wake waliokuwa wamepagawa na show yake jukwaani kunako uwanja wa mpira wa Sam Nujoma. Davido Davido ambaye alipanda Jukwaani na msanii mwenzie kutoka Nigeria, RunTown alijikuta akivutwa na mashabiki wake huku walinzi wa show hiyo wakijitahidi kumchomoa kutoka kwa mashabiki hao. Tayari imeripotiwa kuwa wakati anavutwa na mashabiki hao, wahuni walimvua saa na viatu kitu ambacho kilimfanya ashindwe kuendelea na show.