Posts

Showing posts from October 11, 2018

Kocha wa Taifa Stars Afunguka Kuhusu Figisu Cape Verde

Image
Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars'  Hemed Morocco, amesema wamepokelewa vizuri na hakuna figisu zozote walizofanyiwa mpaka sasa kwenye kambi yao huko nchini Cape Verde. Morocco amebainisha kuwa walipofika jana mchana wakapewa huduma na maelekezo yote ikiwemo uwanja wa kufanyia mazoezi ambao kwa mujibu wa taratibu za FIFA utakiwa kuwa uwanja ambao utachezewa mchezo husika na wao wamefanyiwa hivyo. ''Kiukweli hakuna figisu tangu tulipofika jana, tumepewa uwnja wa taifa ambao tutachezea mechi na ndio tumefanyia mazoezi ya jana jioni, kitu ambacho ni kizuri kwetu kuelekea mchezo huu wa muhimu'', amesema. Mbali na hilo Morocco ambaye pia ni kocha mkuu wa Singida United amesema wachezaji wote wapo vizuri na wana ari ya mchezo wakionesha ushindani mkubwa kwenye mazoezi. Kila mchezaji anajituma sana kwenye mazoezi, ushindani ni mkubwa kila mmoja anaonesha uwezo wake ili kujaribu kuona kama wanaweza kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kw...

Tamko la Kangi Lugola Sakata la Kutekwa kwa Mo Dewji

Image
NancyTheDreamtz Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola amewathibitishia watanzania kulishughulikia kwa haraka na kwa uwezo wa hali ya juu kuhakikisha Mo Dewji anapatikana. Amewaomba watanzania na wana Dar es salaam kushirikiana na polisi katika kutoa taarifa za kiitelijensia kuhakikisha wote waliohusika na utekaji wa mfanyabaishara huyo wanatiwa mbaroni. Amesema watu hao wanalitia doa taifa na Rais wetu kwa ujumla. Makonda akanusha taarifa za kupatikana kwa Mo’ Dewji Lugola amesema hayo kufuatia tukio kubwa lililotokea hapa nchini ambapo watu wasiojulikana alfajiri ya leo wamemteka mfanyabiashara mkubwa Mo Dewji na kumpeleka sehemu zisizojulikana. Mo ametekwa katika hoteli ya Colosseum ambapo alikwa anaenda kwa ajili ya mazoezi, watu wasiojulikana walifyatua risasi na kumuingiza kwa nguvu katika gari yao. Aidha kumekuwa na uvumi juu ya kupatikana kwa Mo Dewji jambo ambalo limekanushwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kusema kuwa bado jeshi la polisi kwa kutumia vyo...

FID Q aeleza mazito aliyoambiwa kuhusu marehemu Pancho Latino ‘alikataa mwili wake kuagwa Leaders’ (+video)

Image
NancyTheDreamtz Rapper FID Q ambaye ni mwanakamati wa mazishi ya marehemu Pancho Latino, amefunguka mambo mazito ambayo ameambiwa na ndugu wa marehemu pamoja na Pancho Latino kabla ya umauti kumkuta siku ya jana. FId Q amesema kuwa ndugu wa marehemu wamemwambia Pancho alikataa katu katu mwili wake kuagwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam.

Navy Kenzo watoboa siri ya maisha ya Pancho kabla ya kukumbwa na umautia (+Video)

Image
NancyTheDreamtz Kundi la muziki la Navy Kenzo wamefunguka mwanzo mwisho wakati wakiongea na waandishi wa habari juu ya maisha ya marehemu Pancho. Moja ya mwanachama wa kundi hilo Producer Nahreel amesema kuwa ” Pancho alishawahi kunambia mbele ya wasanii wengi kabisa kuwa sisi Maproducer hatupati tunachostahili tunafanya kazi kubwa sana ila tunachopata ni kidogo mno”

Producer Manecky afunguka kwa uchungu “hakuna wa kumfananisha na Pancho” (+Video)

Image
NancyTheDreamtz Mwandaaji wa muziki kutoka Tanzania Manecky amefunguka juu ya ukaribu wake na aliyekuwa producer mwenzake aliyeaga dunia maeneo ya Mbudya wakati anaogelea Pancho Latino. Maneckey amesema ” Pancho alikuwa na vitu adimu sana ukimfananisha na Maproducer wa sasa”

Eto’o aeleza kilichomleta Tanzania, akumbuka alivyomfunga Ivo Mapunda miaka 10 iliyopita (Video)

Image
NancyTheDreamtz Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o tayari amewasili Tanzania ambapo kesho atazindua wa kiwanja kilichojengwa na Castle Africa 5 . Related Articles

Harmonize akutana na Meneja wa TI & Travis Scott, uongozi wake waahidi mambo makubwa (+Audio)

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize amekutana na meneja wa wasanii maarufu nchini Marekani, Jason Geter na uongozi wake umezungumzia tukio hilo. Harmonize na Jason Geter Akiongea na Bongo5, Meneja wa Harmonize, Mr Puaz amesema kuwa wapo Marekani kupiga show kwenye baadhi ya miji mbalimbali, lakini pia kupanua wigo wa Bongo Fleva nchini Marekani. Mr Puaz na Jason Geter Mr Puaz amesema kuwa leo amekutana na meneja Jason Geter na wamefanya mazungumzo ya kikazi huku akiwaahidi mashabiki wa Harmonize kukaa mkao wa kula. Jason Geter  kwa sasa anawameneji wasanii wakubwa wawili nchini Marekani ambao ni TI na Travis Scott.

Kamanda Mambosasa awataja waliohusika kumteka mfanyabiashara mkubwa Tanzania Mo Dewij (+Video)

Image
NancyTheDreamtz Taarifa kubwa kabisa zilizoenea kwa sasa ni zile kuwa mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji ,ametekwa leo alfajiri wakati alipokuwa akielekea mazoezini. Kwamujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mo alifika katika hoteli moja ya kifahari katika eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam kama ilivyo ada yake kila siku alfajiri kwaajili ya kufanya mazoezi ya viungo. Hatahivyo, punde aliposhuka tu kwenye gari yake, watu wasiofahamika walijitokeza na kufyatua risasi hewani kisha kumnyakua mfanyabiashara huyo na kutokomea nae kwenye gari lao. Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amezungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa “wamepata taarifa hiyo na wanaifuatilia ingawa waliohusika na utekaji huo wakitajwa kuwa ni wazungu wawili ambao walijifunika nyuso zaona kunvamia wakati anashuka na kufanikiwa kutekeleza tukio hilo ingawa madhumuni ya utekaji bado hatujayajua”