Posts

Showing posts from July 22, 2022

Rais Biden Akutwa na Covid-19, Taarifa Yatikisa Ikulu ya Marekani

Joe Biden Rais wa Marekani RAIS wa Marekani Joe Biden ameripotiwa kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Covid-19 hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani. Rais Biden alikuwa tayari ameshatumia dozi mbili za kujikinga na Covid- 19 aina ya Pfizer muda mchache kabla ya kuingia madarakani ambapo chanjo ya kwanza alichanja mwezi Septemba 2021 na ya pili alichanja mwezi Machi mwaka huu. “Asubuhi ya leo Rais Biden amekutwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 na amechanjwa vizuri ingawa amekumbwa na dalili za maambukizi ya virusi hivyo.” Alisema Msemaji wa Ikulu Karine Jean –Pierre. Biden aripotiwa kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Covid-19 Kwa muda mrefu Ikulu ya Marekani imekuwa ikiendesha shughuli mbalimbali zinazohusisha mikusanyiko ya watu pasipo kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Covid-19. Aidha mnamo Aprili 30, 2022 Rais Biden alihudhuria shughuli yenye mkusanyiko wa watu wengi katika Ikulu ya WhiteHouse akiwa hana tahadhari yoyote ...

Diamond Ajibu Mapigo Tuhuma za P Funk Kwa WCB, Atoa Tamko Zito

Diamond Platnumz akiwa na Rayvanny SUPASTAA wa Bongo Fleva ambaye pia ni Mkurugenzi wa lebo ya Wasafi amekanusha tuhuma za kwamba lebo yake inawanyonya wasanii kama inavyodaiwa na baadhi ya watu huku akisisitiza kuwa lebo yake ndiyo inawanyanyua wasanii wadogo kuwainua na kuwafanya kuwa wasanii wakubwa na matajiri nchini. Kauli hiyo ya Diamond inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Prodcer mkongwe wa Bongo, P Funk Majani kudai kuwa WCB inawakadamiza na kuwadhulumu wasanii wake kwa kuwapa mikataba mibovu yenye nia ya kuwadidimiza kimuziki na kibiashara ili WCB ineemeke. Akihojiwa na DW ya nchini Ujerumani, Mondi amesema; “Muziki ni biashara, sisi katika lebo ya WCB tuliwachukua baadhi ya wasanii wakiwa katika makampuni tayari wakifanya kazini, lakini hawakuwa wakubwa, anapokuja kwetu tunawekeza, tunakifanya kile anachokifanya kiwe kikubwa na kiweze kuingiza fedha na awe mkubwa. Ndio maana wasanii wa Wasafi wanakuwa wakubwa sana. “Inapokuja biashara inakuwa kubwa wengi wa vijana wana...

Jinsi masuala ya tehama yalivyofanyika Wizara ya kilimo Dodoma na Nyandiche Technology&Security Services Tanzania Ltd

Ukizungumzia Masuala ya Tehama Tanzania unapaswa kujua kuwa kuna Vijana wanao jitambua ndani ya Nchi hasa katika kutoa huduma zifuatazo:- 1.Elactrical Fence 2.Access Control 3.Cctv Camera 4.Vehicle system 5.Data Entry in system account ackage's 6.Remote Gate 7.Graphics 8.ICT Solutions 9.Video Door Phone 10.Ld Sensor 11.Web Based Data management 12.Printer na Photocopy Repair Shughuli tajwa hapo juu ni kati ya chachu ya kimaendeleo hasa kwa Vijana Tanzania kwa ujumla kwani inatoa ajira timilifu kwa wahusika wa masuala hayo ya Tehama hapa Nchini kwasasa na kwa mfano hapo chini tunakuletea Video za Kijana ajulikanae kama Arthur Raphael Nyandiche akiwa anafanya kazi ya kutengeneza Printer za Wizara ya kilimo Dodoma Prepared by nyandichethedreamtz