Deus Kaseke Asaini Miaka Miwili Yanga
KATIKA kuhakikisha wanakiboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao, Yanga imemuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo Deus Kaseke. Huyo atakuwa mchezaji wa pili kuongezewa mkataba. Kaseke ni kati ya wachezaji kipenzi cha Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ambaye tangu akabidhiwe kikosi hicho amekuwa akimtumia nyota huyo katika kikosi cha kwanza. Huyo anakuwa mchezaji wa pili kuongezewa mkataba Yanga kati ya hao ambao mikataba imemalizika, mwingine ni Mapinduzi Balama. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Yanga hivi sasa inafanya usajili wake kwa usiri mkubwa na tayari imewaongezea mikataba wachezaji wake ambao Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi amewapendekeza. Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kati ya wachezaji waliongezewa mikataba yupo Kaseke ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.Aliongeza kuwa tofauti na wachezaji wanaoongezewa mikataba, pia mabosi wa timu hiyo wanaendelea na usajili mpya wa kitaifa na kimataifa. ...