JPM Akichukua Fomu NEC, Wasanii 109 Kukesha Uhuru Stadium – Video

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu wa 2020, Dkt. John Pombe Magufuli atachukua Fomu ya Kugombea Urais wiki hii katika ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma.

 

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Agosti 5, 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM (OND) Lumumba Jijini Dar es Salaam. 

“NEC imetutangazia kuanzia leo tunaweza kuchukua fomu kwa ajili ya wagombea wa nafasi ya urais. Mwenyekiti wetu na Rais wetu ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama chetu, Dkt. John Magufuli atachukua fomu wiki hii NEC, Dodoma akiomba dhamana ili akafanye makubwa zaidi kwenye muhula wa pili. Nitawaambia ni siku gani atachukua.

 

“Kampeni tutakazozifanya mwaka huu zitakuwa ni bora zaidi na zitakuwa za kisayansi. Kwa mujibu wa tafiti tuliyoifanya mwezi Juni mwaka huu, tunaingia kwenye uchaguzi tukiwa na mtaji wa wapiga kura milioni 16.8, ambao ni wanachama wa CCM, wapo wengine waliohamia hivi karibuni kabla ya Bunge kuvunjwa kama akina Silinde.
“Agosti 15, 2020 pale Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuna jambo, tutakuwa na tamasha kubwa la ndani la kutambulisha nyimbo za CCM za kabla ya kampeni, wakati wa kampeni na baada ya kampeni (kusherehekea ushindi), kutakuwa na wasanii (mmoja mmoja) 109 na bendi wakiwemo Diamond, Alikiba, Harmnonize, Billnas, Dudu Baya, Pam D, Mesen Selekta, Dulla Makabila, Haitham Kim, Shilole, Snura, n.k. Wataanza saa 4 asubuhi mpaka kesho saa 4,” amesema Polepole.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele