Posts

Showing posts from January 11, 2019

SIMBA CHUNGA HAWA JUMAMOSI TAIFA

Image
NancyTheDreamtz Kikosi cha JS Saoura. KATIKA kitu ambacho Simba watafurahia wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi dhidi ya JS Saoura ni shangwe nzito za mashabiki wao ambao watakuwa wakiongozwa na msemaji wao Haji Manara ambaye atapiga kambi kuzunguka majukwaa ya kawaida. Lakini tathmini ya kiufundi inaonyesha kwamba wapinzani wao kwenye mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, watacheza soka la pasi lakini la kujilinda sana huku wakiwategemea watu watano. Video mbalimbali za timu hiyo zinaonyesha kwamba ikiwa ugenini kwenye mechi za ligi inaweka ukuta mzito na kuacha watu wachache mbele lengo likiwa ni kulazimisha sare au suluhu. Hivyo Simba inapaswa kuwabana kwelikweli. Staili hiyo huenda ikawapa nafasi kubwa Simba ambao wamepania kushambulia kwa nguvu kupitia katikati na pembeni jambo ambalo huenda likaibua shangwe kubwa haswa kutokana na staili mpya ya kushangilia iliyopewa jina la ‘Yes We Can’ chini ya Manara. Waalgeria hao ambao tayari wametanguliza wa...