Posts

Showing posts from September 10, 2018

Esma Azidi Kumkandamiza Mobetto Skendo Ya Uchawi " Tunayajua Mambo Yake Mengi Makubwa Tunalipua Bomu Muda Wowote"

Image
NancyTheDreamtz Dada wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kumtolea povu Hamisa Mobetto na kudai yeye ndio chanzo cha sakata hilo la uchawi kufika mbali. Familia ya Diamond iliingia Kwenye headlines mapema wiki iliyopita baada ya kumtuhumu Mobetto kwa tuhuma za kuwaendea familia yao  kwa mganga. Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda kwenye mahojiano maalum kuhusiana na sakata hilo, Esma alisema amekuwa akizushiwa lawama na matusi kwamba ndiye aliyevujisha ishu hiyo jambo ambalo si kweli. Unajua kama sisi tungekuwa wabaya, basi tungeweka kila kitu kwenye mitandao, lakini kutokana na watu hawaelewi, wanatutukana na kutusema vibaya kwa sababu tu hawajui ukweli wa hili jambo”. Esma alizidi kutiririka na kudai kuwa anawashangaa watu kuwaona wao kama wakosefu na labda hawampendi Hamisa, lakini siyo kweli ni kwa sababu tu mwanamitindo huyo anatengeneza sura ya huruma kwa watu. Watu wanaweza kusema mama yangu ana matatizo, lakini siyo, kwa sababu hata

Huyu Ndie Mchungaji Aliyepigwa Risasi 40 na Majambazi Bila Kupenya Mwilini

Image
NancyTheDreamtz Wakati ulimwengu ukibuni njia ya kuweza kubuni mavazi ambayo yatazuia risasi kutokupenya kiurahisi kwenye mwili wa binadamu, hii ni tofauti kwa Mchungaji wa Kanisa la Grace and Power Prophetic Ministry International, David Elijah kutoka Nigeria ambaye wiki iliyopita amenusurika kifo kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kanisani. Mchungaji David siku ya Ijumaa Septemba 7, 2018 akiwa mjini Awka, Anambra huko Nigeria alikuwa anaenda kanisani kwake akiwa kwenye gari alivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto na kuanza kumfyatulia risasi. Gari hilo lilitobolewa karibia lote kwa risasi lakini mpaka maaskari wanafika eneo la tukio, walimkuta mchungaji David Fulana yake ikiwa yenye matundu ya risasi huku mwili wake ukiwa haujajeruhiwa hata kidogo. Hata hivyo, maaskari hao walimkamata kwa mahojiano zaidi huku wakitahamaki tukio hilo kwamba amewezaje kupona kwenye shambulizi hilo. Tayari Jeshi la Polisi katika jimbo la Anambra limemuachia Mchungaji huyo s

John Makini Awajia Juu Wanaom’beza Mdogo WakeNiya Yake ya Urais

Image
NancyTheDreamtz Kaka wa rapper Nikki wa pili wa kundi la Weusi, Joh Makini amewajia juu wanaomponda na kum’beza mdogo wake, kutokana na uamuzi wa kutangaza nia na ndoto yake ya kuwa Rais. ‘’Ni kitu kizuri kwa mtu kuwa na ndoto kubwa na kitu kilichonisikitisha pale tu Nikki Wa Pili alitangaza ndoto yake kubwa ya kuwa Rais wa Tanzania alikutana na vipingamizi vikubwa kwa watu wengi wakiona kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani inaonyesha ni jinsi gani tuko katika taifa la watu wasio na ndoto, ni kitu kibaya sana lazima uwe na ndoto, lazima uwe na kitu kinachokwambia kwamba siku moja wewe utakuwa mtu fulani na ukiifanyia kazi hiyo ndoto yako utaweza kuifanikisha maana hapa chini ya jua hakuna kinachoshindikana, kwahiyo namtakia kila la heri na baraka zote atimize ndoto zake’’ Alisema John Makini akifanya mahojiano na mtandao wa www.cloudsfm.co.tz

Picha ya Irene Uwoya Yazua Balaa Mtandaoni

Image
NancyTheDreamtz BigieMsanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya amejikuta akiibua mjadala mkubwa mara baada ya kuachia picha ambayo inaonyesha eneo la kifuani likiwa wazi kwa asilimia kubwa. Mremmbo huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuweka picha hiyo ambapo mashabiki wake wamejikuta wakichagia kwa wingi kuliko ilivyo kawaida kuhusu picha hiyo  Picha iliyozua gumzo

Fahamu jiwe la ekari 7 lenye ramani ya bara la Afrika linalotumika katika ibada za kimila Tanzania

Image
NancyTheDreamtz Huwenda umepata kusikia maajabu mengi duniani hebu fahamu na hili, huko Mkoani Njombe Kusini Magharibi mwa nchi ya Tanzania kuna jiwe kubwa kwa jina la Lwiwala lenye ramani ya bara la Afrika. Jiwe hilo la ukubwa ekari 7.8 limejizoelea umaarufu mkubwa kutokana na kuwepo kwa ramani ya bara la Afrika ambayo haijachorwa na mtu. Katika mahojiano yake na Shirika la habari la BBC Mhifadhi Msitu wa Lwiwala, Yuda Masamaki amesema kuwa wakazi wa kijiji hicho hulitumia jiwe hilo katika ibada za kimila. ”Limepewa jina Lwiwala kwa sababu humeremeta nyakati za usiku, baadhi ya wakazi hutumia jiwe hilo kama madhabahu ya ibada zao za kimila,” amesema Yuda Masamaki ambaye ni Mhifadhi Msitu wa Lwiwala. Masamaki ameongeza ”Humu kuna ramani ya Afrika ambayo haijachongwa na wanakijiji, isipokuwa ilitambuliwa na wataalamu.” Jiwe hilo lenye ramani ya Afrika maarufu kama Lwiwala hutembelewa na watalii mbalimbali huku wageni wakitozwa dola 25 za Kimarekani huku wazawa dola mbili pekee.