Posts

Showing posts from May 31, 2023

Hiki Hapa Kikosi Cha Wananchi Kinachokwea Pipa Kuelekea Algeria

KIKOSI cha Wananchi, Young Africans SC kinachokwea pipa kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa fainali ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa Juni 3, 2023. nyandichethedreamtz

Kocha Wa Manchester City Pep Guardiola Atwaa Tuzo Ya Kocha Bora Wa Mwaka Wa LMA

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola. Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka na Chama cha makocha wa Ligi. Hii ni mara ya tatu kwa Guardiola kutwaa Tuzo hiyo inayoitwa ‘Sir Alex Ferguson Award’, iinayopigiwa kura na mameneja ama makocha wa madaraja yote ya ligi nchini England. Mhispania huyo, 52, pia alishinda tuzo ya kocha ama meneja bora wa mwaka wa ligi kuu England baada ya timu yake kunyakua taji la tatu mfululizo na la tano katika misimu sita. Kocha wa Chelsea, Emma Hayes alishinda kwa upande wa Ligi ya Wanawake ya Super League. Ilikuwa tuzo yake ya nne mfululizo na ya sita kwa jumla. Guardiola amekuwa meneja wa tatu kushinda tuzo tatu au zaidi za kocha bora wa mwaka wa LMA, sawa na David Moyes, lakini bado yuko ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson mwenye tuzo 5. City watamenyana na Manchester United katika fainali ya Kombe la FA Jumamosi. Ushindi katika mechi hiyo unaweza kuipa nafasi ya City kushinda makombe matatu

#Exclusive Video: Jokate Afichua Ya Ujauzito Wake, Mtoto Aliyemuokota – ”Ningeweza Kujificha”…

Mkuu Wa Wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo ameweka wazi kuwa anafurahishwa na kitendo cha yeye kuitwa mama kwani ni steji aliyokuwa akiiogopa sana, ila kwa sasa anaongozwa na neno la Mungu na hivyo hana wasiwasi kwani yupo wa kumshindia katika maisha yake. Aidha Jokate ameongeza kuwa suala la yeye kuwa mama au wamama wengine kote duniani ni jambo la kumshukuru Mungu kwani daktari wake mmoja alimueleza kuwa kwa siku moja watu takribani 30 hufika hosptali kutafuta watoto. nyandichethedreamtz

Martha Mwaipaja – UNASEMA NINI (Official Video)

Muimbaji wa Nyimbo za Injili hapa nchini Martha Mwaipaja, Ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la-Unasema Nini. nyandichethedreamtz

Real Madrid Na Man United Zaongoza Orodha Ya Klabu Zenye Thamani Zaidi Duniani

Manchester United ndio klabu yenye thamani kubwa zaidi katika ligi ya Premier, kulingana na orodha iliyotolewa na tovuti ya biashara ya Forbes Jumatano. United, yenye thamani ya $6bn (£4.8bn), ni ya pili kwenye orodha nyuma ya Real Madrid ya Uhispania $6.07bn – mara ya kwanza klabu mbili kuwa juu ya $6bn. Liverpool, Manchester City, Chelsea, Tottenham Hotspur na Arsenal pia wameingia 10 bora. Thamani ya Forbes kwa Manchester United imeongezeka kwa 30% tangu mwaka jana. Klabu hiyo ya Old Trafford iliuzwa na familia ya Glazer mwezi Novemba, huku benki ya Qatar Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani na Ineos Group ya Sir Jim Ratcliffe wakiwasilisha ombi la kuinunua United. Real ilishika nafasi ya kwanza kuanzia 2022 huku ikiongeza thamani yake kwa 19%, huku wapinzani wao Barcelona wakiwa katika nafasi ya tatu wakiwa wameongoza orodha hiyo mwaka 2021. Tangu Forbes waanze kuchapisha orodha ya timu zenye thamani kubwa zaidi za kandanda duniani mwaka 2004, ni Real Madrid na Manchester Unit

Marekani: Baraza La Wawakilishi Lapitisha Mswada Wa Kuongeza Muda Wa Serikali Kukopa Fedha

Kevin McCarthy Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumatano liliidhinisha sheria ya kusimamisha ukomo wa kukopa kwa serikali, hadi mapema mwaka 2025, hatua inayoepusha mzozo wa kisiasa wa Washington, siku tano kabla ya nchi hiyo kufikia wakati ambapo ingekosa pesa za kulipa madeni yake. Katika kura hiyo ya Jumatano, wabunge 314 walipitisha mswada huo dhidi ya 117, walioupinga. Baada ya hapo, mswada huo sasa unaelekea kwenye baraza la Seneti ambapo utapigiwa kura kufikia mwishoni mwa wiki. Endapo utapitishwa na seneti, baraza ambalo linadhibitiwa na Wademokrat kwa wingi wa wajumbe, basi Rais Biden atautia saini na kuwa sheria. Hatua hiyo inasimamisha kiwango cha sasa cha deni la serikali la $31.4 trilioni. Wabunge wa chama cha RepubliKan wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia, wamekosoa makubaliano yaliyofikiwa na Rais Mdemokrat Joe Biden na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mrepublikan Kevin McCarthy kwa kutopunguza vya kutosha, matumizi ya serikali ya siku za usoni, huku baadhi ya