Waziri Lugola Awaondoa Madarakani Maafisa Wa NIDA Mkoa Wa Ruvuma
NancyTheDreamtz Na Mwandishi Wetu, MOHA, Songea. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amemuondoa madarakani Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Ruvuma, Seif Mgonja kwa kosa la kutogawa kwa wananchi Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN), 14,493 tangu Disemba 31, 2019, licha ya kuzalishwa na Makao Makuu na kuletewa ofisini kwake Mjini Songea. Pia Waziri Lugola amemuondoa madarakani Afisa wa NIDA Wilaya ya Namtumbo, Mkoani humo, Thobias Nangalaba kwa uzembe wa kutofika katika kikao chake cha viongozi wa Mkoa na Wilaya, licha ya kupewa taarifa ya kuhudhuria kikao hicho. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Soko Kuu la Manispaa ya Songea Mkoani humo, leo, Waziri Lugola amesema, amewatengua vyeo maafisa wawili hao kwa kucheza na kazi za Serikali, kwa kutojali majukumu yao. “Ndugu wananchi wa Songea, maafisa hawa wamekuwa wakienda kinyume na maagizo ya Serikali la kuwataka waweze kuwakamilishia wananc...